Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- USALAMA

Video ya mauaji huko Tigray yaliweka matatani jeshi la Ethiopia

Video iliyonaswa kupitia simu ya rununu imeanza kufichua siri ya yale yanayojificha katika vita huko Tigray, kaskazini mwa Ethiopia.Uchunguzi wa kina ulioendeshwa na mwandishi wa habari wa uchunguzi kutoka Ethiopia, Zakaria Zelalem,uliochapishwa na gazeti la Uingereza la Daily Telegraph Jumamosi, unaonyesha wanajeshi wa Ethiopia wakitembea huku kijisifu kati ya maiti za raia ambao waliua hivi karibuni.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, akiwa ziarani mjini Pretoria, Afrika kusini January 12 2020
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, akiwa ziarani mjini Pretoria, Afrika kusini January 12 2020 Themba Hadebe/AP Photo
Matangazo ya kibiashara

Video hii ya dakika nne ilikuwa ikizunguka kwenye mitandao kwa siku kadhaa. Kulingana na mwandishi huyo wa habari, toleo kamili ambalo aliweza kuona halivumiliki kutazama.

Kazi ya uainishaji wa mahali pa tukio inaonyesha kwamba mauaji hayo yalitokea katika kitongoji ch Debre Abay, kusini magharibi mwa mji wa Shire.

Katika eneo hilo ndipo wanajeshi wa Ethiopia, wakiwa katika sare zinazotambulika wazi, waliua karibu raia 40, Januari 5.

Kwa upande wa mamlaka nchini Ethiopia, ubalozi wa London tu ndio umeweza kutoa maoni yake. Katika taarifa, ubalozi wa Uingereza umelaumu kuwa video hii ilitumiwa, "nje ya muktadha" na "bila uthibitisho".

Lakini umahidi kufanya uchunguzi na kuchukuwa vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.