Pata taarifa kuu
SUDAN

Walinda amani wa UN wafanya doria ya mwisho Darfur

Walinda amani wa umoja wa Afrika na wale wa umoja wa Mataifa, hivi leo wamefanya doria ya mwisho kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan, hatua iliyoashiria kutamatika rasmi kwa operesheni ya kulinda amani iliyodumu kwa miaka 13.

Walinda amani wa umoja wa Mataifa nchini Sudan kwenye jimbo la Darfur
Walinda amani wa umoja wa Mataifa nchini Sudan kwenye jimbo la Darfur UN Photo/David Manyua
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Octoba kati ya waasi na Serikali, wanajeshi wa Sudan sasa watachukua hatamu ya ulinzi na usalama kwenye eneo hilo, ambako maelfu ya watu wamekufa tangu kuzuka kwa vita kwenye eneo hilo mwaka 2003.

Watu wanaokadiriwa kufikia laki 5 bado wanaishi kwenye kambi za wakimbizi jimboni Darfur.

Mashambulizi kwenye eneo hilo bado yanashuhidiwa na tayari raia wameeleza hofu ikiwa wanajeshi hao wataondoka.

Msemaji wa umoja wa Mataifa, amesema licha ya wanajeshi wa kulinda amani kuondoka, tume ya umoja huo bado itasalia nchini Sudan kuwasaidia raia wa taofa hilo.

Juma lililopita, mapigano ya kikabila yalisababisha watu 15 lkuuawa na wengine mamia kujeruhia.

Juma lililopita, wananchi wa Darfur, ambao wengi bado wanaishi kwenye makambi, walifanya maandamano kupinga walinda amani hao kuondoka.

Mwanzoni mwa mwaka huu baraza la usalama la umoja wa Mataifa liliridhia kutamatishwa kwa operesheni za kulinda amani ifikapo Desemba 31, 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.