Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-TIGRAY

Serikali ya Ethiopia yatangaza kumalizika kwa operesheni za kijeshi huko Tigray

Mamlaka nchini Ethiopia imesema sasa wameanzisha utaratibu wa kisheria dhidi ya viongozi wa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) na misaada ya kibinadamu itawafikia walengwa.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed © Tiksa Negeri / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Addis Ababa inataka kutoa picha ya ushindi ya kampeni yake katika jimbo la Tigray. Hata hivyo ni vigumu kuthibitisha habari hiyo.

Kulingana na mwandishi wetu katika ukanda huo, Sébastien Németh, Serikali ya Addis Ababa inataka kwa sasa kushughulikia utaratibu wa kukamatwa viongozi wa chama cha TPLF, kurejeshwa kwa sheria na utulivu, na pia kuhusu masuala ya misaada ya kibinadamu kwa raia.

Addis Ababa inataka kuandaa zoezi la kuwarudisha nyumbani wakimbizi waliokimbilia nje ya nchi na wale wa ndani, lakini pia kufufua huduma za uchukuzi na mawasiliano, miundombinu iliyoharibiwa na vikosi vya TPLF, kulingana na serikali.

Wakati huo huo serikali ya Addis Ababa inasema operesheni ya kuurejesha kwenye himaya ya serikali kuu mji wa Mekele, siku 10 zilizopita, ilifanyika vizuri bila hata hivyo kuripotiwa hasara yoyote (vifo, majeruhi ya raia au uharibifu wa mali).

Wakaazi wa mji mkuu wa jimbo la Tigray wamesema jiji hilo halina maji, halina umeme, na hakuna huduma ya benki. Mashahidi pia wanasema waliona watu waliouawa na wengine waliojeruhiwa, pamoja na nyumba zilizoharibiwa na makombora.

Siku chache zilizopita, shirika la Msalaba Mwekundi, ICRC, lilitangaza kwamba kuna ripotiwa uhaba wa vifaa vya matibabu katika hospitali kuu ya mji wa Mekele, pamoja na ukosefu wa mifuko ya kuhifadhi miili ya watu waliouawa. Vyanzo kadhaa pia vimebaini kuwepo na visa vya uporaji, vinavyofanywa hasa na askari wa serikali ya Addis Ababa ambao wanashikilia mji huo.

Kikosi kazi kilichoteuliwa na serikali ya Addis Ababa kuhusu Tigray kinatambua visa hivyo, lakini kimebaini kwamba hakuna askari wa serikali ya kuu aliyehusika. Kimebaini kuwepo na ukosefu wa usalama ulioachwa na TPLF kabla ya kuwasili kwa utawala wa mpito ulioteuliwa na bunge katikati mwa mwezi Novemba. Kikosi kazi hiki pia kimebaini kuwepo na wanajeshi wa TPLF wanaovaa nguo za kiraia ambao wanasemekana wamejificha kati ya raia, na kujihusisha na uporaji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.