Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Ethiopia: Vikosi vya TPLF vyaendelea na mapigano katika jumbo al Tigray

Jeshi la Ethiopia, tiifu kwa serikali kuu ya nchi hiyo, limechukua udhibiti wa Mekele, mji mkuu wa jimbo la Tigray.

Mji wa Mekele
Mji wa Mekele Maggie Fick/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tangu wakati huo, hali inaonekana kuwa shwari katika ngome ya Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) baada ya zaidi ya wiki tatu za mapigano dhidi ya serikali kuu.

 

Vikosi vya serikali ya Addis Ababa bado vinawatafuta viongozi wa chama tawala huko Tigray ambao, kwa upande wao, wanasema vita havijaisha na hawajakata tamaa.

 

Vikosi vya TPLF havina nia ya kuweka silaha chini. Debretsion Gebremichael, kiongozi wa chama hicho, amesema bado yuko katika jimbo laTigray, katika eneo lililo karibu na mji wa Mekele. Rais wa jimbo hilo ameahidi kwamba ataendelea kupambana na "wavamizi" ambao anawatuhumu kutekeleza "kampeni ya mauaji ya halaiki".

 

Hata hivyo Bw. Gebremichael ametishia kwamba kwa wakati wowote, kutumia makombora ambayo wanajeshi wake wanayo. "Tuna hakika kwamba tutashinda," ameahidi.

 

Wakati huo huo, vyombo vya habari vilivyo karibu na utawala wa TPFL vimeripoti kwamba vikosi vya kundi hilo vimelidhibiti kwa mara nyingine eneo moja na kuangusha ndege ya kijeshi ya jeshi la serikali ya Addis Ababa.

 

Hata hivyo ni vigumu kuthibitisha habari hivyo kwani jimbo la Tigray limetengwa na ulimwengu baada ya mawasiliano kukakatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.