Pata taarifa kuu
MALI-AQMI-USALAMA

Mali: AQMI yampata kiongozi mpya anayemrithi Abdelmalek Droukdel

Kulingana na tovuti kadhaa maalum, kundi la AQMi lenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda limemteua mmoja wa maafisa wake wakuu kuchukua nafasi ya Abdelmalek Droukdel.

Abdelmalek Droukdel, aliyeuawa, Juni 2020, wakati wa operesheni ya jeshi la Ufaransa kaskazini mwa Mali. (Picha ya kumbukumbu)
Abdelmalek Droukdel, aliyeuawa, Juni 2020, wakati wa operesheni ya jeshi la Ufaransa kaskazini mwa Mali. (Picha ya kumbukumbu) AFP/THOMAS COEX
Matangazo ya kibiashara

Abdelmalek Droukdel aliuawa mwezi Juni mwaka huu, wakati wa operesheni ya jeshi la Ufaransa Kaskazini mwa Mali.

Kiongozi mpya anaitwa Abou Oubéïda Youssef. Ni miongoni mwa maafisa wa kundi hilo wenye ushawishi mkubwa. Mwandishi wetu huko Bamako, Serge Daniel, ametazama video hiyo ikitangaza uteuzi wa kiongozi mpya wa Aqmi.

Video hiyo, iliyorushwa hewani na chombo cha propaganda cha Al-Qaeda katika ukanda wa Magharibi (AQMI), imeweka wazi jina la kiongozi wake mpya: Abu Obeida Youssef Al-Annabi.

Ni afisa zamani wa mwenye shawishi mkubwa katika kamati ya ushauri ya kundi hilo la jihadi. Anajulikana sana kwenye uwanja wa mapigano. Kama mtangulizi wake, Abu Obeida Youssef Al-Annabi ni raia wa Algeria. Picha yake inaonekana kwenye video hiyo, akiwa amevaa nguo nyeupe, akiwa na ndevu nyingi.

Wakati huo huo kundi la AQMI limethibitishal kwa mara nyingine, kifo cha kiongozi wake wa zamani, Abdelmalek Droukdel. Aliuawa mwezi Juni na vikosi vya Ufaransa kaskazini mwa Mali, kwa msaada wa jeshi la Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.