Pata taarifa kuu
MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Mali yaomboleza kifo cha rais wa zamani Amadou Toumani Touré

Rais wa zamani wa Mali Amadou Toumani Touré, ambaye alitawala nchi hiyo kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2012, kabla ya kutimuliwa kupitia mapinduzi ya kijeshi, alifariki dunia usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, akiwa na umri wa miaka 72 , huko Uturuki, ambako alikuwa amepelekwa kwa sababu za kiafya.

Amadou Toumani Touré wakati wa tangazo lake la kujiuzulu Aprili 8, 2012.
Amadou Toumani Touré wakati wa tangazo lake la kujiuzulu Aprili 8, 2012. Guillaume Thibault/RFI
Matangazo ya kibiashara

Rambirambi zinaendelea kumiminika kutoka ulimwenguni kote. Ofisi ya rais wa Mali imetoa rambirambi zake kwa familia ya rais huyo wa zamani. Rais wa sasa, Bah N'Daw, alitoa taarifa ya kupongeza "mmoja wa mashujaa wakubwa katika demokrasia ya Mali" na "ujasiri wa kipekee" ambao "ulisaidia Mali kuwa na taswira yake ya kipekee kisiasa".

Ahmed Mohamed ag Hamani alikuwa mmoja wa mawaziri wakuu wa Amadou Toumani Touré kuanzia mwezi Juni 2002 hadi mwezi Aprili 2004. Kabla ya hapo alikuwa mshirika wa karibu wa Amadou Toumani Touré (ATT). Rafiki aliyeungana na rais wa zamani kwa uhusiano wa kifamilia: "Kwanza alikuwa askari. Askari mkubwa na mzalendo, na jasiri sana. Kama mwanasiasa, alifanya mengi kwa nchi yake, kwa kuboresha maridhiano kwanza, na kwa ujenzi wa nchi yake. Kile ninachoangali kutoka kwake, kama mwanadamu, ni jinsi alivyoheshimu kiumbe mwanadamu, familia yake na pia kwa nchi yake na raia wake. Kwa kweli alifanya mambo mengi ya kusifu. Lakini nilichopenda zaidi ni uaminifu wake ... mimi binafsi nitakumbuka mengi kutoka kwake, " amesema Ahmed Mohamed ag Hamani.

Ahmed Mohamed ag Hamani anakumbuka kuwa rais huyo wa zamani alidhalilishwa kabla ya kuondoka nchini Mali.

"Labda, kwa kuwa yeye ni mtu rahisi sana na mnyenyekevu, kurejea kwake hivi karibuni nchini, na kukaribishwa kwa vifijo na nderemo huko Mopti, labda ilimuosha makosa aliyotuhumiwa na baadhi ya watu ambao walijaribu kumdhalilisha katika nchi yake mwenyewe, " ameongeza Ahmed Mohamed ag Hamani.

Amadou Toumani Touré aliongoza ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo mwaka 1996 na 1997. Pia alikuwa mjumbe maalum wa Koffi Anan mnamo mwaka 2001 nchini humo. Rais wa zamani wa Mali, wakati huo akiwa uhamishoni, alikuwa ameweza kuandaa mazungumzo ya kisiasa kati ya wahusika wa mapinduzi yaliyoshindwa na rais wa zamani Ange-Félix Patassé.

Amadou Toumani Touré pia aliongoza ujumbe wa upatanishi nchini Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.