Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Abiy Ahmed atoa muda wa saa 72 kwa viongozi wa Tigray kujisaimisha

Waziri mkuu wa Ethiopia Abby Ahmed, ametangaza makataa ya saa sabini na mbili 72 kwa vikosi vinavyoongoza mapigano Kaskazini mwa eneo lenye utata la Tigray, kujisalimi kwa serikali.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Desemba 7, 2019.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Desemba 7, 2019. © Tiksa Negeri / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inayojiri wakati majeshi yanayoegemea upande wa serikali ya Ethiopia yakitangaza kuelekea kudhibiti mji kuu wa Mekelle.

“Njia ya uharibifu wenu inakaribia kufikia mwisho na tunawaomba mjisalimishe ndani ya muda wa saa 72 zijazo. Huu ni ujumbe uliotumwa jana Jumapili na Abiy Ahmed kwa viongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF).

Kwa hivyo rais amewasihi kuweka chini silaha. "Mumefikia kwenye hatua ambayo hamna jinsi ya kujikwamua. Chukua nafasi hii ya mwisho kuweza kujisalimisha, " ameongeza.

Saa chache kabla ya tangazo hilo, jeshi la Ethiopia lilionya kwamba shambulio dhidi ya Mékélé linakaribia kutekelezwa. Msemaji wa jeshi alitoa wito kwa wakaazi 500,000 ambao wanaishi katika eneo hilo kuondoka haraka. "mumepewa maagizo ya kujitenga na kundi hilo la waasi, baada ya hapo hakutakuwa na msahama. "

Kwa kujibu tangazo hili kutoka kwa jeshi, Debretsion Gebremichael, mkuu wa vikosi vya TPLF, ameahidi kwamba vikosi vyake vitafanya "mashambulizi makubwa". Shambulio dhidi ya Mékélé halitabadili chochote kwenye uwanja wa mapigano kwa sababu "maadamu wanajeshi bado wapo katika jimbo la Tigray, mapigano hayatakoma, " amesema.

Jumamosi, serikali ilisema jeshi liliteka miji kadhaa kwenye barabara kuelekea Mékélé. Wakati huohuo TPLF ilishutumu vikosi vya jeshi kwa kuua raia wakati wa mashambulizi ya anga katika mji wa Adigrat. Mdai ambayo yamefutiliwa mbali na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.