Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

UNICEF: Watoto 2.3 wahitaji msaada wa dharura Ethiopia

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto duniani la UNICEF limesema mapigano yanayoendelea kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia yamewafanya watoto milioni 2.3 kuhitaji msaada wa dharura, huku maelfu zaidi wakiwa katika hatari na baadhi yao wakiwa wamewapoteza wazazi wao.

Maelfu ya wakimbizi wa Ethiopia waliwasili katika siku za hivi karibuni na kupewa hifadhi katika kambi za muda kwenye kilima cha Hamdayet.
Maelfu ya wakimbizi wa Ethiopia waliwasili katika siku za hivi karibuni na kupewa hifadhi katika kambi za muda kwenye kilima cha Hamdayet. RFI/Eliott Brachet
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, Unicef inasema maelfu ya wakimbizi wanaotoroka mapigano wanaendelea kukimbia ambapo watoto, wanawake na wazee wakiwa ndio waathiriwa wakubwa wa machafuko hayo.

Eneo la Tigray limekabiliwa na mapigano ya umwagaji damu tangu Novemba 4, wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipotangaza uzinduzi wa operesheni za kijeshi dhidi ya serikali ya eneo hilo.

Wiki hii Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi – UNHCR, lilisema kwamba zaidi ya wakimbizi 27,000 walikimbia kutoka Ethiopia na kuingia mashariki mwa Sudan, kufuatia mapigano yanayoendelea eneo la Tigray.

UNHCR insema kwamba idadi hiyo ya wakimbizi ni kubwa zaidi kuwahi kuoekana katika siku za hivi karibuni nchini Sudan.

Kwa kiwango cha wastani, wanawake, watoto na wanaumme 4,000 wanavuka mpaka wa Ethiopia na kuingia Sudan kila siku.

Hali imeendelea kuwa mbaya katika eneo la Tigray tangu serikali ya Ethiopia ilipoanza mashambulizi ya kijeshi wiki mbili zilizopita.

Serikali ya Ethiopia imesema mashambulizi hayo yanatokana na shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Tigray – TPL dhidi ya kambi ya jeshi la serikali.

Maafisa wa UNHCR wamesema kwamba hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya katika eneo la Tigray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.