Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Waasi wa Tigray warusha maroketi katika mji wa Bahir Dar

Shambulio la maroketi lililotekelezwa na vikosi vya waasi huko Tigray katika mji wa Bahir Dar katika mkoa wa Amhara halikusababisha uharibifu wowote, serikali ya katika jimbo hilo imesema leo Ijumaa.

Wanajeshi wa Ethiopia kwenye barabara inayoelekea kwenye mpaka na jimbo la Tigray.
Wanajeshi wa Ethiopia kwenye barabara inayoelekea kwenye mpaka na jimbo la Tigray. AP
Matangazo ya kibiashara

"Kundi haramu la Tigray People's Liberation Front (TPLF) limetekeleza shambulio la maroketi karibu saa 1:40 usiku huko Bahir Dar," ofisi ya mawasiliano ya serikali imesema katika ukurasa wake wa Facebook, na kuongeza "roketi hazikusababisha uharibifu wowote katika mji wa Bahir Dar."

Mzozo kaskazini mwa Ethiopia umeua mamia ya watu katika muda wa wiki mbili, na kusababisha watu 33,000 kuyatoroka makaazi yao na kukimbilia nchini Sudan.

Wengi wameendelea kuhoji uwezo wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed - kiongozi kijana kabisa barani Afrika na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka jana - kudumisha mshikamano wa taifa lake lililogawanyika kikabila.

Chama cha TPLF kilitawala siasa za Ethiopia kwa karibu miaka thelathini, hadi alipoingia madarakani Abiy Ahmed mnamo mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.