Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Mgogoro wa Tigray wahamia Eritrea na Sudan

Mashambulizi ya vikosi vya Tigray People's Liberation Front (TPLF) dhidi ya uwanja wa ndege wa Asmara, mji mkuu wa Eritrea, Novemba 14, 2020, yanaashiria kuongezeka kwa mzozo ambao umelikumba jimbo la kaskazini la Ethiopia kwa siku 12.

Vikosi vya Amhara katika mkoa jirani wa Tigray, Ethiopia, Novemba 9, 2020.
Vikosi vya Amhara katika mkoa jirani wa Tigray, Ethiopia, Novemba 9, 2020. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Debretsion Gebremichael, rais wa serikali katika jimbo laTigray, vikosi vyake vimehusika kwa siku kadhaa katika mzozo dhidi ya Eritrea, pamoja na mapigano dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia.

Mamlaka katika jimbo la Tigray zinashtumu Asmara kwa kusaidia jeshi la Ethiopia. Takriban wapiganaji 25,000 wa vikosi vya TPLF wanaokimbia mapigano wamekimbilia nchini Sudan.

Vikosi vya TPLF vimeimtuhumu Eritrea kwa kuruhusu jeshi la Ethiopia litumie ardhi yake kwa kupitisha wanajeshi wake au ndege zake za kivita.

TPLF inadai pia kwamba jeshi la Eritrea linahusika moja kwa moja katika mapigano ya nchi kavu huko Tigray, "baada ya kutuma maelfu ya wanajeshi wake na magari ya kivita".

Eritrea, inayotawaliwa kwa mkono wa chuma na Issayas Afewerki tangu uhuru wake mnamo mwaka 1993, kwa upande wake imekanusha kuhusika katika mzozo huo.

Ushirikiano kati ya Addis Ababa na Asmara

Eritrea na Ethiopia zilisaini makubaliano ya amani mnamo mwaka 2018, lakini kiongozi wa Eritrea Issayas Afewerki bado anachukia viongozi wa jimbo la Tigray kwa sababu ya jukumu kubwa walilochukua katika vita vikali kati ya nchi hizo kuanzia mwaka1998 hadi mwaka 2000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.