Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia yatekeleza mashambulizi kadhaa katika Jimbo la Tigray

Jeshi la Ethiopia limedai kuwa limefanya mashambulizi ya anga nje kidogo ya mji wa Mekelle, mji mkuu wa Tigray, serikali ya Ethiopia ilitangaza leo Jumanne, wakati mapigano yanaendelea kwa karibu wiki mbili sasa.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. AFP/Monirul BHUIYAN
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pia amesema muda wa siku tatu uliotolewa kwa vikosi vya Tigray na wanamgambo wao kujisalimisha umemalizika.

"Kufuatia kumalizika kwa muda huu, hatua kali ya mwisho ya kurejesha utulivu itafanywa katika siku zijazo," Abiy Ahmed ameandika kwenye mtandao wa Facebook.

Mamlaka katika jimbo la Tigray haujajibu kwa sasa kuhusu tishio hilo la serikali kuu ya Ethiopia.

Usiku wa kumkia Jumatatu serikali ya Ethiopia ilitangaza kwamba vikosi vyake viliukomboa mji wa Alamata mkoani Tigray.

Hayo yakijiri, kiongozi wa jimbo hilo linaloasi la Tigray Debretsion Gebremichael, ameuhimiza Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika kuishutumu serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, kwa kutumia silaha za hali ya juu kiteknolojia zikiwemo ndege zisizokuwa na rubani, wakati wa operesheni yake ya kijeshi ambayo imedumu kwa wiki mbili sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.