Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: mzozo wa Tigray wasababisha vifo kadhaa

Mzozo unaoendelea katika jimbo la Ethiopia wa Tigray, tayari umeua mamia ya watu, vyanzo vya jeshi vimesema leo Jumatatu. Kulingana na moja ya vyanzo hivi, karibu wapiganaji 500 wa vikosi vya Tigray waliuawa na jeshi la Ethiopia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed © Tiksa Negeri / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vitatu vya usalama vinaripoti kwa upande wao kwamba jeshi la serikali lilipoteza mamia ya askari katika mapigano hayo.

Kulingana na shirika la habari la REUTERS ni vigumu kuthibitisha idadi takwimu hizo.

Kulingana na wanadiplomasia, maafisa wa usalama na wafanyakazi wa mashirika ya misaada, mapigano yamesambaa kwenye mpaka kati ya jimbo la Tigray na jimbo la Amhara, ambalo linaunga mkono serikali kuu ya Ethiopia, karibu na mpaka na Sudan na Eritrea.

Siku ya Ijumaa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza kwamba wanajeshi wa serikali kuu ya Addis Ababa waliuweka kwenye himaya yao mji wa Dansha kutoka mikononi mwa vikosi vya Tigrayvya People's Liberation Front (TPLF).

Vikosi vya Tigray vina uzoefu na bado vina idadi kubwa ya vifaa vya kijeshi, wataalam wamebaini kwamba idadi ya wapiganaji wa vikosi vya TPLF katika mkoa huo, ambavyo vinasaidiwa na wanamgambo, inafikia jumla ya 250,000, kulingana na shirika la kimataifa linalojihusisha na kutatua migogoro Ia International Crisis Group 5ICG).

Moja wapo ya hatari kubwa ya mzozo unaoendelea ni kwamba jeshi la Ethiopia litagawanyika kwa misingi ya kikabila na kwamba wanajeshi wa serikali kutoka jimbo la la Tigray wameanza kutoroka jeshi na kujiunga na vikosi vya TPLF, kulingana na wataalamu kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.