Pata taarifa kuu
GUINEA-UN-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Guinea: Wapiga kura Milioni Tano kupiga kumchagua rais wao

Rais Milioni Tano nchini Guinea wanapiga kura kumchagua rais wao mpya, wakati kunaripotiwa mgawanyiko kwenye Tume ya Huru ya uchaguzi nchini humo.

Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu huko Matoto (Conakry) tarehe 22 Machi nchini Guinea.
Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu huko Matoto (Conakry) tarehe 22 Machi nchini Guinea. C. Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wagombea kumi na wawili wanachuana kwenye kinyang'anyiro cha urais, pamoja na rais anayemaliza muda wake, Alpha Condé, ambaye anawania muhula wa tatu unaozozaniwa, na mpinzani wake mkuu Cellou Dalein Diallo. Mambo muhimu ya uchaguzi huu.

Wakati uchaguzi unatarajiwa kufanyika kote nchini, kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, raia wengi wa Guinea walioko ughaibuni hawataweza kupiga kura. Zoezi hilo limepangwa kufanyika katika balozi kumi na moja tu za Guinea barani Afrika, kulingana na chanzo kutoka tume ya uchaguzi. Haitakuwa hivyo nchini Senegal au hata Angola, nchi mbili ambako raia wengi wa Guinea wanaishi.

Suala kuu la uchaguzi huu ni kuwania kwa Alpha Condé kwa muhula wa tatu, au kukabidhiana madaraka ya uongozi wa nchi. Vita hivi, rais Conde, ambaye alibadilisha Katiba wakati wa kura ya maoni yenye utata ili kuweza kugombea tena katika uchaguzi, anatarajia kushinda katika duru ya kwanza.

Atakabiliana na wagombea wengine kumi na mmoja, ikiwa ni pamoja na Cellou Dalein Diallo wa UFDG, mpinzani wake kwa mara ya tatu, ambaye alifanya kampeni kwa kauli mbiu "muda umewadia".

Wagombea wengine maarufu ni Ousmane Kaba wa chama cha PADES, Ousmane Doré, Kabélé Camara au hata Abé Sylla ... na wanawake wawili, Makalé Camara na Makalé Traoré.

Ikiwa Ceni inahakikisha kuwa kila kitu kiko tayari kwa uchaguzi, makamishna wa taasisi hiyo wameelezea mashaka juu ya uaminifu wa mchakato huo na hali ya kutokuaminiana inayotawala katika makao makuu ya vyama vya siasa.

Saa chache kabla ya uchaguzi kuanza, kambi tofauti zinashutumiana kwa kuchochea mvutano kwa kuwatishia wajumbe wao.

Upinzani tayari umetangaza kwamba utatangaza matokeo yake wakati taasisi yenye mamlaka kamili ya kutangaza matokeo ya uchaguzi ni Tume huru ya uchaguzi, CENI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.