Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Guinea: Tume ya uchuguzi Guinea yagawanyika

Wananchi wa Guinea wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wao mpya. Katika kinyang’anyiro hicho, rais anayemaliza muda wake, Alpha Condé, anawania muhula wa tatu baada ya kupitishwa kwa Katiba mpya.

Makao makuu ya CENI huko Conakry, Guinea.
Makao makuu ya CENI huko Conakry, Guinea. DR
Matangazo ya kibiashara

Rais Alpha Condé atachuana na wagombea wengine kumi na mmoja, pamoja na mpinzani wake mkuu Cellou Dalein Diallo.

Kila kitu kinaonekana kuwa tayari lakini usiku wa kuamkia uchaguzi, baadhi ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) wamevunja ukimya wao na kukemea mapungufu katika mchakato wa uchaguzi.

Kulingana na Mamadi 3 Kaba, msemaji wa Tume huru ya uchaguei(CENI), kila kitu kiko tayari kwa uchaguzi wa urais kesho Jumapili.

Kampeni za uchaguzi zilifika tamati jana Ijumaa.

Wakati huo huo maafisa wa usalama wamezuiwa watu kuingia katikati ya jiji kuu Conakry bila kutoa sababu yoyote.

Hali hiyo inashuhudiwa jijini Conakry wakati jana kuliripotiwa mauaji ya afisa wa juu wa Polisi katika kambi ya Jeshi, Mashariki mwa jiji la Conaktry.

Ijumaa wiki maafisa wa polisi walionekana kwa wingi wakipiga doria katikati ya jiji hilo, huku rais Alpha Conde mwenye umri wa miaka 82 akifanya kampeni ya mwisho kuelekea Uchaguzi huo.

Rais Conde anawania urais muhula wa tatu baada ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na kuapa kuwania, licha ya kushuhudia maandamano makubwa. Mpinzani wake mkuu ni Cellou Dalein Diallo, Waziri Mkuu wa zamani mwenye umri wa miaka 68.

Uchaguzi huu unaelezwa kukumbukwa na wasiwasi mkubwa, huku ikihofiwa kuwa, huenda mitandao ya kijamii ikazuiwa siku ya Jumapili. Raia wa nchi hiyo wana hofu kuwa huenda kukatokea machafuko baada ya uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.