Pata taarifa kuu
SUDAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Sudan: Abdallah Hamdok apaza sauti dhidi ya Marekani kuhusu vikwazo

Katika mahojiano na Gazeti la Financial Times yalirushwa hewani Jumapili hii, Oktoba 11, Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok ameitaka Marekani kuondoa vikwazo vinayoikumba Sudan.

Waziri Mkuu Abdallah Hamdok anabaini kwamba vikwazo vya Marekani "vinaitenga" Sudan.
Waziri Mkuu Abdallah Hamdok anabaini kwamba vikwazo vya Marekani "vinaitenga" Sudan. AP / File Photo
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Sudan ameishutumu Marekani kwa "kuzorotesha" uchumi wa nchi hiyo, kwa kuiweka kwenye orodha nyeusi ya nchi zinazounga mkono ugaidi na kukandamiza demokrasia.

Kwa upande wa Waziri Mkuu wa Sudan, nchi yake kuwekwa kwenye orodha nyeusi ya Marekani sio haki. Sio tu kwa sababu imekuwa zaidi ya miaka 20 tangu Osama bin Laden afukuzwe nchini - na kutokana na kumpa hifadhi mnamo miaka ya 1990, hali ambayo ilisababisha vikwazo hivi - lakini pia kwa utawala wa Omar al- Bashir, ambaye alimpa hifadhi kiongozi wa Al-Qaeda wakati huo, ulipinduliwa.

"Wasudan hawajakuwa kamwe magaidi, ilikuwa kazi ya utawala wa zamani," Abdallah Hamdok aameliambia Gazeti la Financial Times. Vikwazo hivi ambavyo "vinaiathiri" Sudan, na kudhoofisha uchumi wake ni "vinasababisha" nchi hii "kutoelekea kwenye njia ya demokrasia".

Hata hivyo Waziri Mkuu wa Sudan amefutilia mbali dhana ya uwezekano wa Khartoum kuitambua Israel kabla ya nchi yake kuondolewa kwenye orodha nyeusi ya Marekani. "Tunataka mada hizi zitenganishwe," Abdallah Hamdok amesema.

Kuhusu hatima ya kimahakama ya dikteta wa zamani Omar al-Bashir, Abdallah Hamdok amesema alizungumza suala hilo na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, juu ya uwezekano wa kuunda "mahakama maalum" nchini Sudan, iitakayoundwa na majaji wa Sudan na ICC. Lakini, amesisitiza kuwa "njia bora itakuwa kurekebisha mfumo wa haki wa Sudan" ili ahukumiwe katika nchi yake.

Omar al-Bashir kwa sasa anashtakiwa huko Khartoum kwa mapinduzi ya mwaka 1989. Lakini ICC bado inamtaka. Inataka kumhukumu kwa uhalifu wa kivita na uhalifu wa mauaji ya kimbari wakati wa vita vya Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.