Pata taarifa kuu
SUDAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani yataka Sudani kuondolewa katika orodha yake nyeusi kabla ya Uchaguzi Mkuu

Kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini Marekani, Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo anafanya jitihada kuhakikisha kuwa Sudan inaondolewa katika nchi zinazofadhili ugaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, hapa, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani, Aprili 29, 2020.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, hapa, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani, Aprili 29, 2020. Andrew Harnik/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Sudan iliorodheshwa na Marekani katika orodha hiyo mwaka 1993, baada ya rais wa zamani Omar al Bashir, kuwapa makao magaidi wa Al Qaeda akiwepo Osama Bin Laden.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, aliomba maseneta wa Marekani kuiondoa Khartoum kwenye orodha ya nchi ambazo Marekani inaona kuwa zinafadhili ugaidi duniani, hatua ambayo ingerahisisha kuimarika kwa hali ya uchumi wa nchi hiyo ambao umedorora.

Akizungumza na Mitch McConnell, kiongozi wa wengi kutoka chama cha Republican katika Bunge la Seneti la Marekani Jumatano wiki iliyopita, Mike Pompeo alibaini kwamba hii ni "fursa ya kipekee kuunga mkono kipindi cha mpito kinachoongozwa na raia nchini Sudan."

Aliomba maseneta kupitisha nakala iliyoandikwa na mjumbe wa chama cha Democratic ,Chris Coons, ifikapo katikati ya mwezi Oktoba. Uchumi wa Sudan unaendelea kudorora tangu Marekani kuchukuwa vikwazo mwaka 1993.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.