Pata taarifa kuu
GUINEA-AMNESTY-SIASA-USALAMA

Ukandamizaji dhidi ya waandamanaji: Amnesty International yaigeukia serikali ya Gunea

Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty International limesema Guinea imeshindwa kuwawajibisha vikosi vya usalama kwa ukandamizaji mbaya wa maandamano dhidi ya serikali tangu mwaka jana.

Maafisa wa polisi wa Guinea wakimkabili mmoja w waandamanaji, Novemba 14, 2019.
Maafisa wa polisi wa Guinea wakimkabili mmoja w waandamanaji, Novemba 14, 2019. CELLOU BINANI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo la haki za binadamu limesema katika ripoti yake kwamba Watu wasiopungua 50 waliuawa wakati wa maandamano dhidi ya Rais Alpha Conde kati ya Oktoba 2019 na Julai 2020 katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi,

Takriban  watu 70 walikamatwa katika kipindi hicho hicho, au na kuwekwa korkoroni kwa kosa tu  la kutumia tu haki yao ya uhuru wa kujieleza au kukusanyika kwa amani.

Ripoti hiyo inakuja kabla ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 18 nchini Guinea, ambapo Conde anawania muhula wa tatu wa urais wenye utata.

Maandamano makubwa dhidi ya uwezekano huo yalianza Oktoba mwaka jana, lakini rais huyo alikaidi upinzani na kushinikiza katiba mpya mwezi Machi, ikimruhusu kuwania muhula wa tatu baada ya kuondoa ukomo wa kuhudumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.