Pata taarifa kuu
GUNIEA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Condé kupeperusha bendera ya chama cha RPG katika uchaguzi wa urais Guinea

Rais wa Guinea anayemaliza muda wake Alpha Condé atawania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 18, chama chake kimesema.

Rais wa Guinea Alpha Condé.
Rais wa Guinea Alpha Condé. WU HONG / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati nia ya Alpha Condé ya kuwania katika uchaguzi wa urais nchini Guinea ilizusha maandamo makubwa kwa miezi kadhaa yaliyosababisha watu kadhaa kuuawa mwaka 2019.

Tofauti na chaguzi mbili za urais zilizopita ambapo Alpha Condé mwenyewe alitangaza kugombea, kwa hivi chama chake cha RPG, na vyama vingine vinavyomuunga mkono ndivyo vimemuomba kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi ujao.

Taarifa ya vyama hivyo ilirushwa kwenye vyombo vya habari vya serikali.

Alpha Condé atawania katika uchaguzi wa urais kama ulivyotaka Mkutano Mkuu wa chama chake uliokutana Agosti 5 na 6.

Katika mkutano huo, wajumbe wote waliafikiana kwamba hakuna mtu mwengine ambaye anaweza kupelekea ushindi wa chama chao ispokuwa rais Condé na hakuna mtu mwengine wa kutetea chama cha RPG kwenye nafasi hiyo bila rais Alpha Condé.

Kwa kujibu ombi hilo, Alpha Condé ameweka masharti: "ikiwa mnataka nikubali pendekezo lenu, inabidi mkubalishe kuwa RPG, chama chetu, kinatakiwa kurudi kuwa kama kile kilichokuwa hapo awali," chama kisichombagua yeyote. "

Hii ndio sababu vyama vya wengi vimewasilisha kwa rais pendekezo la makubaliano juu utekelezaji wa mpango huo.

Kulingana na taarifa hiyo, rais Alpha Condé amekubali ombi la wafuasi wake kuwa mgombea wao katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 18.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.