Pata taarifa kuu
GUINEA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Watu kadhaa wauawa katika vurugu za uchaguzi Guinea

Machafuko yaliyoibuka wakati wa kura ya maoni ya Katiba na uchaguzi wa wabunge vikifanyika Jumapili Machi 22 yaligharimu maisha ya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa nchini Guinea.

Makabiliano yalizuka kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji katika baadhi ya maeneo ya mji wa Conakry yenye wafausi wengi wa upinzani wa Katiba mpya, Machi 22.
Makabiliano yalizuka kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji katika baadhi ya maeneo ya mji wa Conakry yenye wafausi wengi wa upinzani wa Katiba mpya, Machi 22. C. Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Upinzani ambao ulisusia zoezi hilo ambalo lilipingwa na Jumuiya ya kimataifa unakusudia kuzuia muhula wa tatu wa rais Alpha Condé.

Watu kumi ndio waliuawa katika machafuko hayo, kwa mujibu wa vuguvugu linaodai kulinda katiba ya nchi (FNDC) kwa siku moja tu ya Jumapili.

Hata hivyo wizara ya usalama imebaini kwamba watu wanne ndio waliuawa kwa siku ya jana ikiwa ni pamoja na wawili katika ghasia, mmoja kufuatia ajali na mwengine kufuatia mshtuko wa moyo, bila maelezo zaidi.

Taarifa hiyo ya wizara ya usalama imeongeza kuwa maafisa 9 kutoka kitengo maalum cha usalama wa uchaguzi, pamoja na maafisa 7 wa polisi, walijeruhiwa vibaya, wakati vuguvugu linalodai kulinda katika ya nchi (FNDC) limetangaza kwamba wafuasi wake kadhaa wamejeruhiwa kwa risasi.

Waandamanaji walishambulia vituo vya kupigia kura, waliharibu na kuchoma vifaa vya uchaguzi katika miji kadhaa nchini na katika maeneo ya mji wa Conakry yenye wafuasi wengi wa upinzani, kwa mlujibu wa Wizara ya Usalama.

Watu kadhaa wamekamatwa kwa makosa ya kuhusika katika machafuko na khatarisha usalama wa raia, kumiliki na kutumia silaha za moto kinyume cha sheria, uharibifu wa mali ya umma, kuchoma moto vifaa vya uchaguzi, kupiga na kufanya uasi dhidi ya serikali, wizara ya usalama imeongeza.

Hayo yanajiri wakati vuguvugu la FNDC limetoa wito kwa wafuasi wake kuendelea na maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.