Pata taarifa kuu
DRC-CODECO-USALAMA

DRC: Kundi la CODECO lahusishwa katika utovu wa usalama Banyali Kilo, Ituri

Miezi ya hivi karibuni, eneo la Banyali Kilo lililoko kwenye mji wa Djugu jimboni Ituri Mashariki lwa DRC, limeendelea kushuhudia mashambulizi yanayotekelezwa na waasi wa CODECO.

Gari la jeshi la Umoja wa Mataifa likipiga doria katika eneo la Djugu, mkoani Ituri, Machi 2018.
Gari la jeshi la Umoja wa Mataifa likipiga doria katika eneo la Djugu, mkoani Ituri, Machi 2018. ALEX MCBRIDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya wakaazi wa eneo hilo pamoja na wawakilishi wa serikali wamelazimika kuyakimbia makwao kwa hofu ya kushambuliwa, licha ya jeshi kusema kuwa inadhibiti hali ya usalama.

Kundi la Codeco limeendelea kunyooshewa kidole cha lawama kuhusima na vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na uporaji katika mkoa wa Ituri.

Shirika la Kimatiafa la kutatua migogoro la International Crisis Group katika ripoti yake mwezi uliopita, lilisema tangu mwaka 2017 utovu wa usalama katika mkoa wa Ituri, umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 na maelfu kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.