Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Upinzani wa Lamuka waandamana, polisi yakabiliana na waandamanaji Kinshasa

Maelfu ya wafuasi wa muungano wa kisiasa wa Lamuka wameandamana katika jimbo kadhaa za DRC Kupinga mpango wa ma rekebisho wa mfumo wa mahakama na uteuzi wa Ronsard Malonda, kuwa mwenyekiti watume huru ya uchaguzi CENI.

Maandamano ya wafuasi wa muungano wa vyama vya upinzani LAMUKA.
Maandamano ya wafuasi wa muungano wa vyama vya upinzani LAMUKA. REUTERS/Benoit Nyemba
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamekabiliana na waandamanaji, huko Kinshasa, kinara wa upinzani Jean Pierre Bemba aliongoza maandamano hayo. Toka Kinshasa Freddy Tendilonge ametuma ripoti ifuatayo

Wafuasi wa muungano wa vyama vya upinzani wa Lamuka na washirika wake pamoja na wanaharakati wanaotetea demokrasia, walimiminika mitaani jijini Kinshasa Jumatatu wiki hii, kupinga uteuzi wa Ronsard Malonda kama mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchunguzi (CENI). Wakidai kuwa Bw Malonda ni mshirika wa karibu na raïs wa zamani Joseph Kabila, ambaye aliteuliwa kwenye nafasi ya mashirika ya kiraia.

“Tutaendelea hadi siku Ceni itakuwa huru na mpaka siku tutasikia kwamba bwana Ronsard Malonda ametenguliwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa CENI. Mtu ambae alitetea wizi naye ni mwizi, “ Espoir  Ndabazi, mmoja kati ya waandamanaji amesema.

“Hatupende huo mchezo, hapana kabisa, tumesema Kabila hatukutaki tena” , Emmanuel Kyala mwanadamanaji mwengine amebaini.

Barabara kuu ya Lumuba ilijaa umati wa wafuasi kutoka vyama vinavyojumuika katika muungao Lamuka na washirika wake amboa waliongozwa na Jean Pierre Bemba moja wa viongozi wa Lamuka. Lakini muda mchache baadaye polisi waliwatawanya kwa mabomu ya machozi na Jean-Pierre Bemba haraka nyumbani alisafirishwa mara moja nyumbani kwake, huku baadhi ya wafuasi wakijeruhiwa.

“Viongozi ambao wamesimamia operesheni hio nadhani walikutana na ujumbe wa  raia. Wanapaswa tu kueshemu jinsi sheria ya CENI inasema kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wa tumehiyo. Kumepaswa kuwa na makubaliano kati ya wanamemba wa vyama vya kiraia, vya kiisiasa kutoka upinzani, lakini yote  yametekelezwa kwa njia isiyo halali, “ amesema Jean-Pierre Bemba.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika maandamano hayo ya Lamuka, yalifanyika katika majimbo kadhaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.