Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Uteuzi wa Ronsard Malonda: Maandamano ya wafuasi wa UDPS yatawanywa na polisi

Polisi jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesambaratisha maandamano ya wafuasi wa chama cha rais Tshisekedi, cha UDPS baada ya kujaribu kuandamana kupinga uteuzi wa Ronsard Malonda kama mwenyekiti wa Tume Huru yaUchaguzi, CENI

Maandamano ya awali dhidi ya uteuzi wa Ronsard Malonda kama mwenyekiti wa CENI, Jumamosi Julai 4, 2020 huko Kinshasa.
Maandamano ya awali dhidi ya uteuzi wa Ronsard Malonda kama mwenyekiti wa CENI, Jumamosi Julai 4, 2020 huko Kinshasa. RFI/Pascal Mulegwa
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa chama cha UDPS na vyama vingine washirika wametaka kuandamana pia dhidi ya mapendekezo ya miswada ya sheria ya mageuzi ya mahakama iliyoletwa na kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila, ambayo inaviti vingikatika Baraza la Wawakilishi na Bunge la Seneti.

 

Maelfu ya wafuasi wa vyama hivyo walikuwa wamekusanyika mbele ya makao makuu ya Bunge la tiafa, Alhamisi hii asubuhi.

 

Hata hivyo walijikuta wakitawanywa na maafisa wa polisi ambao walilazimika kutumia gesi ya machozi.

Hayo yamejiri wakati serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani Gilbert Kankonde ilipiga marufuku maandamano yote yaliyotarajiwa kuanza leo kupinga uteuzi wa Ronsard Malonda kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya uchaguzi CENI nchini humo.

Hatua ya Bunge la taifa nchini DRC kumteua Ronsard Malonda kuwa mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi (CENI) inaendelea kuzua mvutano nchini DRC.

Chama cha UDPS kinashtumu mshirika wake madarakani FCC kusababisha hali hiyo, kwa kwa kujivunia wingi wa viti katika Bunge.

Kufuatia uteuzi huu mungano madaraki (CASH na FCC) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umegawanika. Chama cha UDPS kimefutilia mbali uteuzi wa Ronsard Malond kama mwenyekiti wa Ceni, kikisema kuwa "utaratibu uliotumiwa na FCC kumteua mgombea wake katika nafasi ya asasi za kiraia ni wa aibu".

Kwa upande wa chama hicho cha rais, mshirika wake madarakani hutumia "mabavu" kwa kutaka kuvunja sheria kwa mambo ambayo yanahitaji makubaliano ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.