Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Abiy aahidi kuwakamata waliohusika na mauaji ya mwanamuziki maarufu Ethiopia

Maafisa wa usalama nchini Ethiopia walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwazuia maelfu ya waombolezaji waliokuwa wamejitokeza kushiriki katika mazishi ya mwanamuziki Hachalu Hundessa, aliyeuawa wiki kwa kupigwa risasi na kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya watu 90 baada ya makabiliano na Polisi.

Wengi kama yeye walikimbilia uhamishoni kwa kuhofia kuteswa lakini Hachalu Hundessa aliamua kusalia nchini kuwahimiza vijana wapiganie haki yao.
Wengi kama yeye walikimbilia uhamishoni kwa kuhofia kuteswa lakini Hachalu Hundessa aliamua kusalia nchini kuwahimiza vijana wapiganie haki yao. Capture d'écran Youtube
Matangazo ya kibiashara

Polisi pamoja na wanajeshi walionekana mapema leo wakipiga doria katika mji wa Ambo, kuzuia mkusanyiko wa watu baada ya waombolezaji wachache kuruhusiwa kuingia uwanjani.

Licha ya purukushani hiyo, mwanamuziki huyo alizikwa na ibada ya mazishi ilioneshwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Jimbo la Oromo.

Santu Demisew Diro, mke wa mwanamiziki huyo aliyeimba nyimbo za kuwahamasisha jamii ya Oromia ambayo watu wake wamekuwa wakilalamika kutengwa na serikali jijini Addis Ababa, ameitaka serikali kujenga mnara jiini Addis Ababa kwa ajili ya kumbukumbuku ya mume wake.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed ambaye anatokea jamii hiyo kubwa ya Oromo amwataka raia wa nchi hiyo kuendelea kuwa kitu kimoja, huku akiahidi kuwa serikali yake itahakikisha kuwa waliomuua mwanamuziki huyo ambaye alikuwa mfungwa wa kisiasa wanapatikana na kuchukuliwa hatua kali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.