Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Mauaji ya wanamuziki Ethiopia: Abiy Ahmed alaani jaribio la 'kuhujumu usalama'

Hali ya usalama imerejea nchini Ethiopia, baada ya maandamano mabaya yaliyosababishwa na mauaji ya mwanamuziki maarufu na mwanaharakati anayetetea haki za watu kutoka jamii ya Oromo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (picha ya kumbukumbu).
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Kumera Gemechu
Matangazo ya kibiashara

Mwili wa mwanamuziki maarufu Hachalu Hundessa umesafirishwa katika mji alikozaliwa wa Ambo, ambapo mazishi yake yamepangwa kufanyika Alhamisi Julai 2.

Katika hotuba yake kwenye runinga Jumanne jioni, Abiy Ahmed hakuwataja wale ambao alikuwa akilenga kwa kulaani kuuawa kwa kiongozi wa vijana kutoka jamii ya Oromo. Mauaji ya Hachalu Hundessa, amesema, "yalitekelezwa na kuchochewa na maadui wa ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuhujumu usalama wa taifa na kutuzuia kumaliza mambo tuliyoanza kuyatekeleza". Maana yake inaweza kulenga Misri na washiriki wake, na inaelezea bwawa kubwa Grand Renaissance lililojengwa na Ethiopia, ambalo limezua mvutano mkubwa kati ya mataifa matatu, Ethiopia, Misri na Sudan.

Wakati huo huo mkuu wa polisi wa Ethiopia amesema kuwa "watuhumiwa kadhaa" wamekamatwa na kwamba mwanamuziki aliuawa akiwa katika gari lake, wakati wa operesheni "iliyoandaliwa vizuri". Amesema, lengo lilikuwa "kuitumbukiza" nchi katika "machafuko".

Maandamano ya Jumanne yalikuwa mabaya. Msemaji wa polisi wa Jimbo la Oromiya amebaini kwamba watu 50 waliuawa, ikiwa ni pamoja na afisa mmoja wa polisi katika mji mkuu. Afisa huyo wa polisi anadaiwa kuwa aliuawakatika makabiliano na walinzi wa mwanasiasa wa upinzani kutoka jamii ya Oromo Jawar Mohamed, ambaye amekamatwa na walinzi wake na mmoja wa viongozi wa chama chake, Bekele Gerba.

Mabomu matatu pia yameripotiwa kulipuka wakati wa makabiliano katika mji mkuu wa Ethiopia. Na kwa mara ya kwanza, sanamu kadhaa za watawala wa zamani wa Ethiopia zimeharibiwa na vijana wenye hasira kutoka jamii ya Oromo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.