Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SUDANI-MSRI-NILE-USHIRILIANO

Misri, Sudan na Ethiopia zafikia makubaliano kuhusu bwawa la al-Nahdhah

Ofisi ya rais wa Misri imetangaza kwamba Misri, Ethiopia na Sudan wamekubaliana kuahirisha zoezi la kujaza maji katika bwawa kubwa lililojengwa na Ethiopia kwenye mto Nile, hali ambayo ilikuwa imezua mvutano mkubwa kati ya nchi hizo tatu.

Ethiopia ilianza ujenzi wa bwawa la al-Nahdhah Aprili 2011 na kwa mujibu wa ratiba ya awali, utumiaji wa maji yake ulikuwa uanze mwaka 2017, lakini ukaahirishwa kutokana na tofauti kubwa zilizojitokeza kati ya nchi hiyo na Misri na Sudan.
Ethiopia ilianza ujenzi wa bwawa la al-Nahdhah Aprili 2011 na kwa mujibu wa ratiba ya awali, utumiaji wa maji yake ulikuwa uanze mwaka 2017, lakini ukaahirishwa kutokana na tofauti kubwa zilizojitokeza kati ya nchi hiyo na Misri na Sudan. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

"Makubaliano ya mwisho ya kisheria ya kuzuia hatua kutoka upande mmoja, pamoja na kujaza maji katika bwawa, yatatumwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili yaweze kujadiliwa katika kikao chake cha Jumatatu kuhusu suala la Bwawa kubwa al-Nahdhah, "imebaini Ofisi ya rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi.

Viongozi kutoka nchi wanachama wa kamati ya uongozi ya Umoja wa Afrika (AU) wamehudhuria kikao cha marais wa nchi hizo tatu.

Kwa upande wake msemaji wa ofisi ya rais wa Misri, Bassam Radhi, amesema kuwa nchi hizo tatu zimekubaliana kujiepusha na uchukuaji hatua yoyote ya upande mmoja ikiwemo kutumia maji ya bwawa la al-Nahdhah kabla ya kufikiwa mwafaka kamili na kwamba madhumuni ya msimamo huo wa nchi hizo tatu yatabainishwa katika kikao cha siku ya Jumatatu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika upande mwingine, Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok alisema katika taarifa kwamba "ilikubaliwa kwamba zoezi la kujaza maji katika bwawa hilo litaahirishwa hadi kufikiwa makubaliano".

“Imeafikiwa kwamba utumizi wa maji ya bwawa la al-Nahdhah uanze baada ya kusainiwa makubaliano kati ya nchi hizo, “Hamdok ameongeza.

Ethiopia ilianza ujenzi wa bwawa la al-Nahdhah Aprili 2011 na kwa mujibu wa ratiba ya awali, utumiaji wa maji yake ulikuwa uanze mwaka 2017, lakini ukaahirishwa kutokana na tofauti kubwa zilizojitokeza kati ya nchi hiyo na Misri na Sudan.

Misri inaitakidi kuwa ujenzi wa bwawa hilo utakuwa na taathira hasi kwa mgao wake wa kila mwaka wa maji ya Mto Nile, lakini Ethiopia inasema, ujenzi huo hautasababisha madhara yoyote kwa nchi hiyo na Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.