Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SUDANI-MSRI-NILE-USHIRILIANO

Ujenzi wa bwawa kwenye Mto Nile: Mzozo waendelea kutokota kati ya mataifa jirani

Mvutano unaendelea kati ya nchi zinazotumia maji ya Mto Nile, ambapo shughuli za ujenzi wa bwawa la umeme wa zinazoendeshwa na Ethiopia zimezua mvutano mkubwa na nchi zingine mbili zinazotumia maji ya mto huo, ambazo ni Misri na Sudan.

Ujenzi wa bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia utakuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme barani Afrika.
Ujenzi wa bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia utakuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme barani Afrika. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Suala hili linajadiliwa Jumanne wiki hii katika mkutano wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu, kwa ombi la Cairo. Nchi zinazotumia maji ya mto huo, zinabaini kuwa zinategemea kila upande mto huo.

Siku ya Jumamosi Juni 20, 2020 Misri ilisema ililiomba baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati mzozo wake wa muda mrefu na Ethiopia kuhusu bwawa la umeme katika mto Nile.

Hatua ya Misri inakuja siku chache baada ya duru ya mazungumzo kati ya Misri, Ethiopia na Sudan kuhusiana na bwawa hilo kumalizika bila ya kupatikana muafaka. Addis Ababa inatarajia kuanza kulijaza bwawa hilo la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) mwezi ujao.

Mto wa nile ni muhimu kwa Misri. Misri inategemea maji ya mto Nile kwa 97% .

Ujenzi wa bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia utakuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme barani Afrika.

Ujenzi huo ulianza mwaka 2011 kaskazini mwa Ethiopia ambapo maji yatakayotumika ni 85% ya maji yanayotiririka kutoka mto Nile.

Hata hivyo ujenzi huo umesababisha kuwepo kwa mzozo kati ya Misri na Ethiopia, huku Sudan pia ikihusishwa.

Mradi huu mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme utakaogharimu dola bilioni nne unategemewa kuzalisha kiwango kikubwa cha umeme barani Afrika.

Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kutoa umeme wa nguvu ya 'megawatts' 6,000.

Ethiopia inakabiliwa na tatizo la uhaba wa umeme, zaidi ya 65% ya idadi ya watu nchini humo hawajaunganishiwa umeme.

Kihistoria, Misri inategemea kwa kiwango kikubwa cha maji ya mto Nile hivyo kama mfumo wa maji hayo utaathirika basi nchi nzima itaathirika.

Makubaliano ya mwaka 1929 iliwapa Misri na Sudan haki ya maji ya mto wote wa Nile.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.