Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA-USALAMA

Waziri Mkuu wa Ethiopia aongezwa muda wa kusalia madarakani

Bunge la Ethiopia limepitisha kuongezwa muda wa kusalia madarakani kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu, kuahirishwa kufuatia janga la Corona.

Abiy aliingia madarakani mwanamo 2018.
Abiy aliingia madarakani mwanamo 2018. AFP/Monirul BHUIYAN
Matangazo ya kibiashara

Wabunge 114 walipiga kura kuidhinisha hatua hiyo, huku wanne wakipinga, kura zilizopigwa siku mbili baada ya Spika wa bunge, Keria Ibrahim kujiuzulu akisema  Waziri Mkuu Ahmed anapanga kusalia madarakani kutumia mlango wa nyuma.

Uchaguzi utaendelea katika kipindi hicho mara baada ya mamlaka za afya kueleza kwamba janga la virusi vya corona sio tena kitisho cha kiafya kwa umma, amesema msemaji wa bunge Gebru Gebreslassie.

Kuongezewa muda kwa Abiy kunaweza kusababisha mvutano zaidi kati ya serikali na chama cha Tigray People's Liberation, TPLF, kinachopinga maamuzi yaliyofikiwa mwezi Machi ya kusogeza mbele uchaguzi kutokana na janga la Corona.

Chama cha Tigray People's Liberation, TPLF, kimetishia kufanya uchaguzi wake katika jimbo la Tigray, ambako ni nyumbani mwa makundi ya kikabila yenye ushawishi mkubwa nchini Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.