Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA-USALAMA

Mvutano waibuka kati ya serikali ya Ethiopia na utawala wa Jimbo la Tigray kuhusu uchaguzi

Serikali ya Jimbo la Tigray, Kaskazini mashariki mwa Ethiopia imesema kuwa itaandaa uchaguzi unaolenga kuchagua bunge jipya, licha ya kuwa serikali ya Addis-Ababa ilichukua uamuzi wa kuahirisha uchaguzi huo katika ngazi ya kitaifa.

Debretsion Gebremichael, kiongozi wa chama cha Tigray People's Liberation Front akizungumza wakati wa mkutano wa chama Januari 4, 2020 huko Mekelle (picha ya kumbukumbu).
Debretsion Gebremichael, kiongozi wa chama cha Tigray People's Liberation Front akizungumza wakati wa mkutano wa chama Januari 4, 2020 huko Mekelle (picha ya kumbukumbu). EDUARDO SOTERAS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni sehemu ya mwisho ya mvutano kati ya serikali kuu na chama kinachotawala jimbo hilo linalopakana na Eritrea, ambacho kilitolewa madarakani baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi mwaka 2018.

Kamati tendaji ya chama cha Tigray People's Liberation Front ilikutana mwishoni mwa wiki iliyopita na taarifa yake ilimlenga Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed kwanza, na Chama chake kipya cha Prosperity, chama alichoanzisha mwenyewe, ambacho wanasiasa wa chama cha Tigray People's Liberation Front walikataa kijiunga nacho.

Pia taarifa hiyo ilipinga uchaguzi wa wabunge, uliokuwa umepangwa kufanyika Agosti 29, kusogezwa mbele kutokana na ugonjwa hatari wa Cpvid-19, wakisema kuwa ni "kinyume na katiba ya nchi". Uamuzi huo ulichukuliwa na serikali ya Addis-Ababa.

Suala hili halijtatuliwa katika ngazi ya kitaifa. Suala la kumalizika kwa muhula wa wabunge ifikapo Oktoba 10, na kusalia madarakani kwa viongozi ikiwa kutakuwa na taasisi za mpito, leo liko mikononi mwa Baraza kuu la Bunge na jopo la majaji wa mahakama ya Katiba. uamuzi wa taasisi hizo mbili unatarajiwa kutolewa katika siku zijazo.

Hata hivyo chama cha Tigray People's Liberation Front kimetangaza kwamba uchaguzi utafanyika "kwa wakati, kwa mujibu wa Katiba". Jambo ambalo linapingwa na Tume huru ya Uchaguzi ikibani kwamba yao peke ndio ina mamlaka ya kuitisha uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.