Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-AQMI-USALAMA

Jeshi la Ufaransa lathibitisha kifo cha Abdelmalek Droukdel

Kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abdelmalek Droukdel na "wasaidizi wake kadhaa", waliuawa na askari wa Ufaransa Juni 3 kaskazini mwa Mali.

Askari wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane nchini Mali, Julai 2019 (picha ya kumbukumbu).
Askari wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane nchini Mali, Julai 2019 (picha ya kumbukumbu). Reuters/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Operesheni ya kijeshi ambayo ilisababisha kifo chake ilifanyika katika mkoa wa Tessalit, karibu na mpaka wa Algeria.

Alhamisi hii asubuhi, makao makuu ya jeshi la Ufaransa yametoa maelezo zaidi kuhusu operesheni hiyo.

Operesheni iliyoendeshwa Juni 3 Kaskazini mwa Mali na vikosi vya Ufaransa kwa msaada wa washirika wao ilisababisha kifo cha kiongozi (Amir) wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Aqmi Abdelmalek Droukdel, Waziri wa Jeshi Florence Parly wa Ufaransa alitangaza Ijumaa Juni 5 kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Operesheni hiyo ilitekelezwa Kaskazini mwa eneo la Adrar des Ifoghas, kilomita 80 Mashariki mwa Tessalit, karibu na mpaka na Algeria.

Habari hii ilikuwa bado haijathibitishwa kwa sababu shambulizi hilo dhidi ya kiongozi huyo lilitekelezwa na ndege isiyokuwa na rubani ya jeshi la anga la Ufaransa, likifuatiwa na mashambulizi ya helikopta. Watu 5 , kiongozi wa kundi la Aqmi Abdelmalek Droukdel na wasaidizi wake, ikiwa ni pamoja na afisa mwandamizi anayehusika hususani na propaganda katika kundi la Aqmi waliuawa katika mashambulizi hayo.

"Vikosi vya Ufaransa vilivyotumwa katika operesheni vinathibitisha kwamba leo jkiongozi wa kijihadi Abdelmalek Droukdel ameangamizwa" amebaini Kanali Frédéric Barbry, msemaji wa makao makuu ya majeshi ya Ufaransa, na kuongeza kuwa wameweza kumamata mmoja wa wapiganaji hao. Mmoja wa wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi alijisalimisha bila kupigana.

Abdelmalek Droukdel ni kiongozi wa kijihadi katika ukanda huo, na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kwenye makundi kadhaa ya jihadi katika ukanda wa Sahel, pamoja na kundi la JNIM au GSIM kwa Kifaransa, kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu.

Kulingana na chanzo rasmi, vipimo vya damu vilivanywa na kubaini kwamba mmoja kati ya watu waliouawa ni Abdelmalek Droukdel.

Mwishoni mwa mwaka wa 2018, jeshi la Ufaransa lilitangaza kifo cha Amadou Koufa, kiongozi wa kundi la katiba Macina, kabla ya mtu huyo kuonekana tena kwenye video miezi michache baadaye.

Ufaransa kwa sasa inasubiri kuona iwapo kundi hilo la Aqmi litatangaza kifo cha kiongozi wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.