Pata taarifa kuu
SAHEL-AMNESTY-MAUAJI-USALAMA

Ripoti: Watu 200 wauawa kati ya mwezi Februari na Aprili Sahel

Raia 200 waliuawa na vikosi vya ulinzi na usalama katika ukanda wa Sahel kati ya mwezi Februari na Aprili, kulingana na ripoti ya shirika la kimataifa ya Haki za binadamu Amnesty International, iliyotolewa leo Jumatano.

Visa vya unyanyasaji katika ukanda wa Sahel vimeongezeka.
Visa vya unyanyasaji katika ukanda wa Sahel vimeongezeka. AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii inatolewa siku kadhaa baada ya shirika lingine la haki za binadamu nchini humo la Tabital Pulaaku, kulishtumu jeshi la Mali kwa kufanya mauaji ya raia katikati mwa nchi hiyo. Mauaji ambayo hayajathibitishwa na mamlaka nchini Mali.

Ukatili huu (mauaji au visa vya watu kutoweka) sio wa kwanza kuripotiwa nchini Mali, Niger na Burkina Faso. Kulingana na Amnesty International, watu wasiopungua 199 waliuawa na vikosi vya ulinzi na usalama kati ya mwezi Februari na Aprili 2020.

"Takwimu hizi ni makisio ya chini," Ousmane Diallo, mtafiti wa shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International amesema. Tangu mkutano wa Pau, uliofanyika mnamo mwezi Januari kati ya nchi za G5 Sahel na Ufaransa, "tuna ushahidi tosha kuhusu ukatli huo. Hii mara nyingi huonekana katika ukiukwaji unaofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama, "amebaini Ousmane Diallo, mwandishi wa ripoti hiyo.

Kwa kweli kuna shinikizo la kisiasa kutoka kwa majeshi ya Mali, Niger na Burkina na hii inaelezwa kwa mfumo wa operesheni zao ambapo hawaheshimu hata haki za binadamu na sheria za kimataifa kuhusu haki kibinadamu ...Ousmane Diallo, mtafiti katika Amnesty International ameongeza.

Ripoti ya Aprili ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, MiNUSMA, pia inavishtumu vikosi vya Mali na Niger kwa machafuko dhidi ya raia.

Visa vya unyanyasaji katika ukanda wa Sahel vimeongezeka. nchini Mali, siku ya Ijumaa, shirika la haki za binadamu la Tabital Pulaaku, lilishtumu jeshi la Mali, kulingana na ushuhuda kuhusika kwa kuteketeza kwa moto kijiji kimpka kinachopatikana katikati mwa Mali. Mamlaka ilisema inatambua idadi ya vifo 29 vya wanakijiji. Lakini kwa mujibu wa taarifa, "wahusika hawakujulikana".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.