Pata taarifa kuu
LESOTHO-SIASA-HAKI

Waziri mkuu wa Lesotho anayekabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe wa zamani aondoka nchini

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane anayekabiliwa na mashitaka ya kumuua mke wake wa kwanza Lipolelo Thabane hakufika mahakamani, wakati alitakiwa kufika mahakamani leo Ijumaa kusikilizwa kuhusu tuhuma hizo.

Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane amekaa na mkewe Maesaiah Thabane wakati kuapishwa kwake huko Maseru Juni 16 Juni 2017.
Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane amekaa na mkewe Maesaiah Thabane wakati kuapishwa kwake huko Maseru Juni 16 Juni 2017. Photo: Samson Motikoe/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkewe wa kwanza bwana Thabane,58. alipigwa risasi katika mji mkuu wa Maseru, siku mbili kabla ya bwana Thabane kuwa waziri mkuu 2017.

"Hakufika mahakamani, alienda Afrika kusini kwa matibabu , na vipimo hivyo ni vya mara kwa mara" , katibu wake Thabo Thakalekoala ameliambia shirika lahabari la AFP.

Wakati huo huo naibu kamishna wa polisi Paseka Mokete amewaambia waandishi wa habari kwamba watasubiri ili kuendelea na kesi hiyo hadi atakaporudi nchini.

“Hatuwezi kwa sasa kusema kwamba alikiuka agizo la mahakama, ” Paseka Mokete ameongeza.

Mapema mwezi Februari 2020, mke mpya wa Waziri Mkuu, Maesaiah, alishtakiwa rasmi kwa mauaji ya mke mwenzana sasa yuko nje kwa dhamana ya dola 67.

Pia ameshtakiwa na jaribio la mauaji ya rafikiye Thato Sibolla ambaye alikuwa na Lipoleo wakati wa tukio hilo la mauaji na anatarajiwa kuwa shahidi mkuu katika mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.