Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-BARKHANE-USALAMA

Askari wa pili wa Barkhane kutoka Ufaransa auawa nchini Mali

Kikosi cha askari wa Ufaransa Barkhane kimewapoteza askari wawili ndani ya siku nne nchini Mali. Kévin Clément, askari wa jeshi la Ufaransa mwenye umri wa miaka 21, "aliuawa katika vita" Jumatatu Mei 4 wakati wa operesheni dhidi ya makundi yenye silaha nchini Mali, rais wa Ufaransa amesema.

Kevin Clément, askari wa Ufaransa aliyeuawa nchini Mali, Mei 4, 2020.
Kevin Clément, askari wa Ufaransa aliyeuawa nchini Mali, Mei 4, 2020. Handout / FRENCH ARMY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kévin Clément ni askari wa pili kuuawa ndani ya siku nne katika kikosi cha askari wa Ufaransa cha Barkhane katika ukanda wa Sahel.

Kévin Clément, alikuwa nchini Mali tangu mwezi Februari mwaka huu. Kifo chake kimefanya idadi ya askari 43 wa Ufaransa waliuawa katika ukanda wa Sahel tangu Ufaransa kuingilia kati kijeshi katika ukanda huo mwaka 2013, kulingana na takwimu zilizotolewa makao makuu ya jeshi la Ufaransa.

Rais Emmanuel Macron "anatoa heshima kubwa kwa askari aliyejitolea kutetea taifa lake nje ya nchi," imesema taarifa kutoka Ikulu ya raia, Elysée. "Rais anapongeza na anaunga mkono askari wa Ufaransa waliotumwa katika ukanda wa Saheli" na "msaada wa Ufaransa kwa nchi za G5 Sahel" (Mali, Niger, Chad, Mauritania, Burkina Faso).

"Licha ya vifo hivyo Ufaransa itaendelea kuunda mkono amani na usalama katika maeneo hayo na hatutakata tamaa hadi mwisho, " amesema Waziri wa Jeshi Florence Parly.

Hivi karibuni idadi ya askari wa kikosi cha Barkhane iliongezwa kutoka askari 4,500 hadi 5,100. Paris inatarajia kwamba idadi hiyo itwezesha kikosi hicho kuyaangamiza makundi ya kijihadi ambayo yaliongeza mashambulizi katika miezi ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.