Pata taarifa kuu
DRC-VIRUNGA-FDLR-USALAMA

Watu zaidi ya 17 waangamia katika katika Hifadhi ya Wanyama ya Virunga DRC

Watu zaidi ya kumi na saba wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika shambuliolililotokea katika Hifadhi ya Wanyama ya Virunga Kaskazini Mashariki mwa DRC.

Hifadhi ya Taifa ya Wanyama ya Virunga karibu na Rutshuru, Juni 17, 2014 (picha ya kumbukumbu).
Hifadhi ya Taifa ya Wanyama ya Virunga karibu na Rutshuru, Juni 17, 2014 (picha ya kumbukumbu). Junior D. Kannah / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea kilomita 40 kutoka mji wa Goma, katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Walinzi kumi na tatu wa Hifadhi ya Wanayama ya Virunga na raia wanne waliuawa papo hapo, kwa mujibu wa mamlaka ya Hifadhi ya Wanyama nchini DRC (ICCN).

ICCN pia imebaini kwamba walinzi watatu wa hifadhi hiyo pamoja na raia sita walijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.

Cosma Wilungula, mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo, amelihusisha kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda la FDLR kwa shambulio hilo.

"Wapiganaji zaidi ya sitini wa kundi la FDLR ndio walitekeleza shambulio hilo la kinyama", amesema Bw. Wilungula.

Siku ya Ijumaa asubuhi, katika eneo la Rumangabo, Mashariki mwa nchi, kundi la watu wenye silaha walishambulia mojawapo ya magari yaliyokuwa yakisafiri kati ya Goma na Rutshuru kusafirisha chakula. Timu za ICCN zinajaribu kulinda usalama wao kwa sababu zinalengwa katika eneo hilo la hifadhi, ameongeza Bw. Wilungula. Ameelezea mazingira ya usalama mdogo katika eneo hilo, kwa sababu ya uwepo wa makundi kadhaa ya watu wenye silaha.

"Timu ya watu wapatao kumi na tano wametumwa ili kulinda usalama wa raia na kusaidia msafara wa magari. Kulikuwa na vitisho kwa muda mrefu, " amebaini mkurugenzi mkuu wa ICCN.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.