Pata taarifa kuu
DRC-DJUGU-USALAMA

DRC: Watu 13 wauawa katika shambulio la wanamgambo wa CODECO Djugu

Eneo la Djugu, katika Mkoa wa Ituri, Kaskazini, Mashariki mwa DRC, linaendelea kukabiliwa na hali ya sintofahamu, wakati kundi la wanamgambo la CODECO linaendelea kuhujumu wakazi wa eneo hilo.

Askari wa jeshi la Umoja wa mataifa wakipiga kambi katika eneo la Lita huko Djugu, Ituri Machi 27, 2018.
Askari wa jeshi la Umoja wa mataifa wakipiga kambi katika eneo la Lita huko Djugu, Ituri Machi 27, 2018. ALEX MCBRIDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu kumi na watatu waliuawa katika shambulio jipya Alhamisi, Aprili 23, na wanamgambo wa kundi la CODECO, katika vijiji vya Sakoko na Samangoli, katika jimbo la Djugu, mkoani Ituri.

Kulingana na vyanzo kutoka eneo hilo, ilikuwa saa sita mchana ambapo watu wenye silaha kutoka kundi la wanamgambo la CODECO walivamia vijiji vya Sakoko na Samangoli, vijiji viwili vinavyopatikana kilomita hamsini na mji wenye madini wa Lisey, kaskazini magharibi mwa Bunia.

Lengo la shambulizi hilo ni kulipiza kisasi vifo vya wanamgambo wenzao wawili, waliouawa usiku wa Jumatano Aprili 22 na vijana wa vijiji hivyo, vyanzo rasmi vimebaini.

Vyanzo hivyo pia vimesema kuwa watu saba, wakiwemo watoto watatu na watu wazima wanne, waliuawa kwa risasi na kwa mapanga.

Msemaji wa jeshi huko Ituri, Luteni Jules Ngongo, ambaye amethibitisha vifo vya raia hao katika shambulio hilo, amesema kuwa watu hao waliuawa kwa risasi wakati vikosi vya serikali kutoka Lisey vinaingilia kati kumtimua adui.

Hata hivyo Luteni Jules Ngongo amesema wauaji sita waliuawa katika urushianaji wa risasi, huku akiongeza kuwa hali imethibitiwa na jeshi la FARDC.

Mji huo wenye madini wa Lisey umekuwa ukikabiliwa kwa siku kadhaa na visa kadhaa vya ukosefu wa usalama, kufuatia kuwepo kwa makundi ya watu wenye silaha ambao wanashambulia raia na vikosi vya serikali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.