Pata taarifa kuu
MISRI-MAREKANI-CORONA-AFYA-USHIRIKIANO

Coronavirus: Misri yatuma msaada wa matibabu nchini Marekani

Misri imetuma kwa ndege vifaa vya matibabu nchini Marekani kusaidia nchi hiyo katika mapambano dhidi ya janga la Covid-19, ikiwa ni msaada wa kibinadamu kutoka nchi hii ambayo hupokea msaada muhimu kutoka Marekani, shirika la Habari la AFP limeandika.

Katika hospitali ya Bronx-Liban katika eneo la Bronx huko New York, Marekani, Aprili 2, 2020.
Katika hospitali ya Bronx-Liban katika eneo la Bronx huko New York, Marekani, Aprili 2, 2020. REUTERS/Brendan Mcdermid
Matangazo ya kibiashara

Misri kwa miaka mingi ni mshirika muhimu wa Marekani. Msaada wa jeshi wa Marekani kwa Cairo ni kama dola bilioni 1.3 kwa mwaka.

Picha za vifa vya matibabu vilivyohifadhiwa katika masanduku yenye maandishi "kutoka kwa raia wa Misri kwenda kwa raia wa Marekani Amerika", kwa lugha ya Kiingereza na Kiarabu, zilizopakizwa kwenye ndege ya mizigo ya kijeshi, zimerushwa kwa video kutoka ofisi ya rais.

Ndege hiyo ilitua kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Andrews karibu na Washington, amebaini Dutcht Ruppersberger, kiongozi wa kidemocrats wa kundi linaloendeleza uhusiano na Misiri katika Baraza la Wawakilishi.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba karibu mask 200,000 na vifuniko 48,000 vya viato, kwa mujibu wa Ruppersberger.

"Hii ndio sababu diplomasia ya kimataifa na kuimarika kwa uhusiano na washirika wetu kama Misri ni muhimu, sio tu wakati wa shida lakini kila siku," Ruppersberger ameandika kwenye mtandao wa Twitter.

Balozi wa Markani nchini Misri, Jonathan Cohen pia amekaribisha msaada huo "muhimu".

Misiri imerrekodi vifo 250 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19 huku ikiwa na visa vya 3,300 vya maambukizi kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), huku Marekani ikithibitisha vifo 45,000 vilivyotokana na Covid-19.

Uamuzi huu wa kutuma msaadawa matibabu nchini marekani umekosolewa huko Misiri, ambapo theluthi moja ya raia wa nchi hiyo wanaishi kwa dola 1.5 au chini ya kiwango hicho kwa siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.