Pata taarifa kuu
CONGO-YHOMBI-SIASA

Rais wa zamani wa Congo-Brazzaville Yhombi Opango afariki dunia

Rais wa zamani wa Congo-Brazzaville, Jacques Joachim Yhombi Opango, ambaye alitawala nchi hiyo kati ya mwaka 1977 na 1979, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Rais wa zamani wa Congo-Brazzaville, Jacques Joachim Yhombi Opango, amefariki dunia jijini Paris.
Rais wa zamani wa Congo-Brazzaville, Jacques Joachim Yhombi Opango, amefariki dunia jijini Paris. youtube.com
Matangazo ya kibiashara

Kifo chake kilitokea Jumatatu Machi 30 nchini Ufaransa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 akiwa na umri wa miaka 81, familia yake imesema.

Hali ya afya ya rais huyo wa zamani wa Congo-Brazzaville ilikuwa imezorota hivi karibuni, na kumlazimu kuishi mbali na nchi yake, nchini Ufaransa hasa, kwa mujibu wa familia yake. Aalikuwa akiishi nchini Ufaransa na Congo-Brazzaville tangu kumalizika kwa muda wake wa kuishi ukimbizini mwaka 2007.

"Baba yangu, rais wa zamani Yhombi Opango, alifariki dunia Jumatatu mchana katika hospitali ya Neuilly-sur-Seine karibu na Paris. Alikuwa mwathirika wa ugonjwa wa Corona, "mtoto wake Jean-Jacques Yhombi Opango ameliambia shirika la Habari la AFP kwa simu. Taarifa hiyo ilithibitishwa baadaye jioni na televisheni ya serikali ya Congo-Brazzaville, Télé-Congo.

Jacques Joachim Yhombi Opango alizaliwa mwaka 1939 huko Cuvette, Kaskazini mwa Congo-Brazzaville. Yhombi Opango, ambaye alikuwa afisa wa zamani, alichukuwa madaraka mara tu baada ya mauaji ya kuhuzunisha ya Rais Marien Ngouabi (1968-1977).

Jacques Joachim Yhombi Opango aliongoza Congo-Brazzaville kwa miaka miwili tu kabla ya kutimuliwa madarakani na Waziri wake wa Ulinzi, Rais wa sasa Denis Sassou Nguesso, kutoka mkoa wa Cuvette.

Hata hivyo rais Jacques Joachim Yhombi Opango alikamatwa kufungwa kwa kipindi cha miaka 10, kabla ya kuachiliwa huru muda mfupi kabla ya mkutano wa kitaifa wa mwaka 1991 ambao ulifungua ukurasa mpya kwa nchi kwa kuanzishwa mfumo wa vyama vingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.