Pata taarifa kuu
CONGO-SIASA

Sassou Nguesso ateuliwa kuwania katika uchaguzi wa urais Congo-Brazzaville

Rais wa Congo-Brazzaville Denis Sassou Nguesso ameteuliwa tena cna chama chake cha PCT kuwania urais mwaka 2021. Uamuzi huu umefanywa na wajumbe wa chama hicho zaidi ya 2,500 katika mkutano mkuu wa chama hicho.

Rais wa Congo-Brazzaville Denis Sassou Nguesso.
Rais wa Congo-Brazzaville Denis Sassou Nguesso. REUTERS/Anis Mili/Files
Matangazo ya kibiashara

Nguesso mwenye umri wa miaka 76, amekuwa kiongozi aliyetawala kwa miaka mingi taifa hilo la Afrika ya Kati.

Wakati wa uamuazi huo, wajumbe wa chama hicho walisema kuwa, hatua ya kutaka rais Nguesso kuendelea kuongoza ni kwa sababu wanataka mwendelezo wa maendeleo na mabadiliko ambayo ameleta katika taifa hilo ambalo hata hivyo, wananchi wengi wote ni maskini.

Katiba ya nchi hiyo, inamruhusu kiongozi huyo kuwania tena urais mwaka ujao na mara ya mwisho mwaka 2026.

Vyama vya upinzani, vikiongozwa na UPADS vimenasema hawaamini kuwa kutakuwa na mazingira mazuri ya kufanikisha uchaguzi utakaokuwa huru na haki mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.