Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU- SIASA-URAIS

Raia wa Guinea Bissau wapiga kura kumchagua rais

Wapiga kura nchini Guinea Bissau wamekuwa wakipiga kura kumchagua rais katika mzunguko wa pili uliowakutanisha waliokuwa Mawaziri Wakuu wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Raia wa Guinea Bissau Desemba 29 2019
Raia wa Guinea Bissau Desemba 29 2019 REUTERS/Christophe Van Der Perre
Matangazo ya kibiashara

Rais wa sasa Jose Mario Vaz alishindwa kumaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili katika mzunguko wa kwanza na sasa baada ya zoezi la siku ya Jumapili, anatarajiwa kuondoka madarakani.

Wanaowania nafasi hiyo ni Domingos Simoes Pereira, mwenye umri wa miaka 56 anayepambana na Umaro Cissoko Embalo, mwenye umri wa miaka 47.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema, ushindani utakuwa ni mkali sana kati ya wawili hao na yeyote anaweza kuibuka mshindi.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa wiki ijayo.

Guinea-Bissau ni koloni la zamani la Ureno, ni nchi ndogo maskini ya magharibi mwa Afrika yenye watu Milioni moja na nusu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.