Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Mvutano na wasiwasi vyaongezeka kabla ya uchaguzi wa Machi 1 Guinea

Hali ya wasiwasi na mvutano vimeendelea kutanda nchini Guinea wakati nchi hiyo ikijiandalia uchaguzi wa wabunge na kura ya maoni kuhusu Katiba ya nchi hiyo Jumapili hii Machi 1.

Bango la uchaguzi la chama cha RPG lililoharibiwa huko Conakry, Februari 23, 2020.
Bango la uchaguzi la chama cha RPG lililoharibiwa huko Conakry, Februari 23, 2020. C. Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mvutano umeongezeka katika kambi tofauti za kisiasa wakati upinzani ukitishia kufanya kilio chini ya uwezo wao ili kuzuia uchaguzi huo usifanyiki. Hali ambayo imesababisha nchi hiyo kuwa katika hali ya sintofahamu, huku raia na mashirika mbalimbali ya kiraia wakiingiliwa na wasiwasi mkubwa.

Kwa upande mmoja, baadhi ya wanasiasa wa upinzani wametoa wito wa kushambuliwa kwa vifaa vya uchaguzi na vituo vya kupigia kura. Upande wa chama tawala wametoa wito wa kuwashambulia wale watakaothubutu kutekeleza mashambulizi dhidi ya vifaa vya uchaguzi na vituo vya kupigia kur.

"Hali hii na kauli zinazotolewa na wanasiasa zinatia wasiwasi," amesema Alseiny Sall kutoka shirika la Haki za Binadamu nchini Guinea huku akibaini kwamba kauli hizo zinazoendelea zinachochea machafuko na chuki kwenye mitandao ya kijamii.

Mahakama ya Katiba imetupilia mbali rufaa zote zilizowasilishwa na upinzani. Viongozi wa kidini wameshindwa kupatanisha pande hizo zinazokinzana, kwa mujibu wa Kabinet Fofana, kutoka shirika la Sayansi za Siasa nchini Guinea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.