Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Guinea: Uchaguzi wa wabunge waahirishwa hadi Machi 1

Uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika Februari 16 nchini Guinea umeahirishwa hadi Machi 1, kulingana na sheria ya Rais Alpha Condé iliyosomwa Jumatatu jioni kwenye runinga ya taifa.

Rais wa Guinea, Alpha Condé akipiga kura huko Conakry katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Rais wa Guinea, Alpha Condé akipiga kura huko Conakry katika uchaguzi wa serikali za mitaa. CELLOU BINANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Alpha Condé ametoa sheria ya kuahirisha tarehe ya uchaguzi wa wabunge, uliyopangwa awali kufanyika Februari 16, 2020, hadi wiki mbili zijazo, sheria ambayo haikuwashangaza wengi.

Mambo kadhaa yanaeleza sababu za kuahirishwa kwa uchaguzi huo: vyama vikuu vya upinzani vilitoa wito kwa wafuasi wao kususia uchaguzi huo, ikifuatiwa na kujiondoa kwa maafisa saba wa tume ya uchaguzi, CENI, wakipinga dhidi ya usimamizi mbovu wa mchakato wa uchaguzi.

Sababu nyingine: viongozi wa dini waliomba watawala wasimamishe maandalizi ya uchaguzi wa wabunge hadi wakati ambapo wadau wote katika mchakato huo watakapokutana kwa maandalizi ya uchaguzi huru, wa wazi, wa haki, wa kuaminika na usiyombagua yeyote.

Kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge kwa mara ya pili katika kipindi kisichopungua miezi 3, ni dhahiri kwamba Tume ya uchaguzi, CENI, inakabiliwa na matatizo ya kuandaa vema kalenda yake ya uchaguzi, wamebaini waangalizi.

Kulingana na waangalizi hao walio karibu na taasisi hiyo, CENI inakabiliwa sio tu na matatizo ya kifedha na kiufundi, lakini pia na matatizo yanayohusiana na rasilimali watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.