Pata taarifa kuu
GUINEA-ICC-SIASA-USALAMA

Mwendesha Mashtaka wa ICC aonya dhidi kuongeza kwa machafuko Guinea

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) Fatou Bensouda, ameonya wale wote wanaohusika na kuongezeka kwa machafuko nchini Guinea.

Rais wa Guinea, Alpha Condé akivaa shati ya rangi ya blu akiwa katikati ya wafuasi wake waliokuja kumuunga mkono, wakati wa maandamano ya Oktoba 31, 2019.
Rais wa Guinea, Alpha Condé akivaa shati ya rangi ya blu akiwa katikati ya wafuasi wake waliokuja kumuunga mkono, wakati wa maandamano ya Oktoba 31, 2019. C. Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Fatou Bensouda ameitaka serikali na upinzani kuanza tena mazungumzo baada ya maandamano mabaya kuwahi kutokea katika nchi hiyo ndogo maskini barani Afrika.

Mvutano mkubwa unaendelea kuikumba Guinea baada ya wiki kadhaa za maandamano yaliyoandaliwa na upinzaji ambao unamshtumu Rais Alpha Condé kutaka kuwania muhula wa tatu.

Makao makuu ya serikali ya Guinea.
Makao makuu ya serikali ya Guinea. RFI/Charlotte Idrac

"Kufuatia ripoti za matukio kadhaa ya machafuko nchini Guinea katika wiki chache zilizopita, natoa wito kwa viongozi wote na wafuasi wao wajiepushe na vurugu na waanze mazungumzo ili kukomesha hali ya uhasama inayoendelea nchini humo," amesema Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda.

"Yeyote anayetenda, kuamuru, kuhamasisha, kuhimiza au kuchangia kwa njia yoyote kutenda uhalifu wa wazi ... atakabiliwa na mashtaka kwenye mahkama za Guinea au ICC," Fatou Bensouda ameonya.

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Fatou Bensouda.
Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Fatou Bensouda. ICC-CPI

Kwa jumla, raia wasiopungua 16 na afisa mmoja wa polisi wameuawa katika maandamano makubwa ambayo Guinea - nchi ndogo, maskini yenye wakaazi milioni 13 - inaendelea kukabiliana nayo tangu Oktoba 14. Watu wengi wamejeruhiwa, na wengine kadhaa wamekamatwa na kuhukumiwa.

Katiba ya Guinea inaweka kikomo cha mihula miwili kwa rais madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.