Pata taarifa kuu
LIBYA-UTURUKI-USALAMA

Libya yaendelea kukumbwa na mgogoro wa kivita

Bunge la Uturuki linatarajia kuamuwa hii leo kuhusu muswada uliowakilishwa bungeni na rais wa nchi hiyo Recep Tayep Erdogan kutuma rasmi wanajeshi nchini Libya kwa ajili ya kuisaidia serikali inayo kubalika na Jumuiya ya kimataifa ya Fayez el-Sarraj dhidi ya vikosi vya Khalifa Haftar.

Mapigano yaendelea kupamba moto Libya.
Mapigano yaendelea kupamba moto Libya. AFP / LNA WAR INFORMATION DIVISION
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo tayari Uturuki imewatuma askari mamluki wa Syria nchini Libya.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Ghassan Salamé amekuwa akituhumu uingiliaji wa mataifa ya kigeni katika mzozo wa Libya, lakini pia kutoheshimu vikwazo vya silaha zinazo ingizwa nchini Libya ambapo hivi karibuni Uturuki imeipa Libya silaha, ikiwemo ndege zisizokuwa na rubani, huku Uturuki ikiwatuma askari nchini humo.

Watafiti wanaona kuwa askari mamluki wanaokwenda Libya ambao wametumwa na Uturuki ni wale waliokuwa wakipambana vita nchini syria dhidi ya rais Bashar Al Assad.

Hofu imeendelea kutanda kuhusu mzozo huo wa Libya ambayo kwa sasa ina serikali mbili, moja dhaifu inayoungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa na ile inayoungwa mkono na Halifa Haftar ambae majeshi yake yanapambana kuuteka mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.