Pata taarifa kuu
UTURUKI-LIBYA-USALAMA-USHIRIKIANO

Uturuki kupeleka vikosi nchini Libya

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake iko tayari kutuma wanajeshi wake nchini Libya kwa ombi la Tripoli. Recep Tayyip ametoa kauli hiyo mbele ya maafisa wa chama cha AKP. Zoezi hilo la kutuma wanajeshi nchini Libya limepangwa kuanza mapema mwezi Januari.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. REUTERS/Bernadett Szabo
Matangazo ya kibiashara

Erdogan amesema bunge la Uturuki litajadili na kupiga kura katika muda wa hadi wiki inayokuja kuamua kuhusu ombi hilo na kuongeza serikali yake itawasilisha muswada wa kupeleka vikosi Uturuki nchini Libya.

Ni jambo la kawaida, lakini ni sheria nchini Uturuki: muswada wa kutuma vikosi nje ya nchi unapaswa kupelekwa mbele ya Bunge. Utaratibu uliotumika kila mwaka kwa nchi ya Syria. Nakala hiyo itawasilishwa Januari 7 na kupigwa kura Januari 8 au 9, serikali ya Ankara imebaini.

"Tutaunga mkono kwa njia zote serikali ya Tripoli, ambayo inakabiliana na mashambulizi ya jenerali muasi,' ameongeza Rais Erdogan, akimaanisha Jenerali Haftar, anayeungwa mkono na Saudi Arabia na Misri.

Uturuki na Libya pia zilitiliana saini mkataba kuhusu eneo la bahari ya Mediterrania ambayo yote pamoja na ule wa ushrikiano wa kijeshi ilikabiliwa na ukosoaji kutoka kanda hiyo na pande nyingine za ulimwengu.

Utawala wa waziri mkuu Sarraj umekabiliwa na uchokozi tangu mnamo mwezi April kutoka serikali hasimu ya upande wa mashariki na vikosi vinavyoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar, ambaye anajaribu kuchukua udhibiti wa mji mkuu, Tripoli.

Januari 8, Vladimir Putin atakuwa nchini Uturuki, ziara iliyopangwa kwa muda mrefu. Rais wa Urusi atashiriki katika hafla ya uzinduzi wa bomba la mafuta la TurkStream, bomba linalounganisha Urusi na China kupitia Bahari Nyeusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.