Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya atangaza vita vya kuteka Tripoli

Kiongozi wa wapiganaji wa upinzani nchini Libya Khalifa Haftar ametangaza vita vya kuliteka jiji kuu Tripoli. Tangazo la hivi punde, limekuja, baada ya kuanza harakati hizi miezi minane iliyopita na sasa amewaagiza wapiganaji wake kusonga mbele na kudhibiti Tripoli.

Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya.
Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, vikosi vya Haftar vimekuwa vikikabiliana na wanajeshi wa serikali ya umoja wa kitaifa, wanaotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Mapema wiki hii Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema kwamba nchi yake iko tayari kutuma wanajeshi nchini Libya. Ankara inatarajia kuimarisha msaada wake wa kijeshi kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya inayoongozwa na Fayez el-Sarraj, ilisem ataarifa hiyo kutoka ofisi ya rais wa Uturuki.

Kauli hiyo inakuja baada ya makubaliano ya hivi karibuni yaliyotiliwa saini kati ya pande hizo mbili.

Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha siku mbili Recep Tayyip Erdogan akieka wazi nia yake ya kutuma viukosi vya kijeshi kusaidia serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya, ambayo inapigana na vikosi vya mbabe wa kivita Mashariki mwa nchi hiyo, Marshal Khalifa Haftar.

Rais wa Uturuki alisema yuko tayari kutuma wanajeshi nchini Libya, ikiwa Libya "itatoa ombi kama hilo".

Urusi imekuwa ikihusishwa kuunga mkono mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya Marshal Khalifa Haftar.

Hata hivyo Urusi imeendelea kukanusha madai kuwa, wanajeshi wake wameendelea kumuunga mkono wapiganaji wa upinzani Khalifa Haftar, ambaye kuanzia mwezi Aprili, amekuwa akijaribu kudhibiti jiji kuu Tripoli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.