Pata taarifa kuu
UTURUKI-LIBYA-USALAMA-USHIRIKIANO

Uturuki yasema iko tayari kutuma wanajeshi kusaidia Tripoli

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kwamba nchi yake iko tayari kutuma wanajeshi nchini Libya. Ankara inatarajia kuimarisha msaada wake wa kijeshi kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya inayoongozwa na Fayez el-Sarraj.

Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha siku mbili Recep Tayyip Erdogan akielezea hoja yake ya kutuma wanajeshi ili kusaidia serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli (picha ya kumbukumbu).
Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha siku mbili Recep Tayyip Erdogan akielezea hoja yake ya kutuma wanajeshi ili kusaidia serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli (picha ya kumbukumbu). © REUTERS/Bernadett Szabo
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo inakuja baada ya makubaliano ya hivi karibuni yaliyotiliwa saini kati ya pande hizo mbili.

Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha siku mbili Recep Tayyip Erdogan akieka wazi nia yake ya kutuma viukosi vya kijeshi kusaidia serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya, ambayo inapigana na vikosi vya mbabe wa kivita Mashariki mwa nchi hiyo, Marshal Khalifa Haftar.

Rais wa Uturuki amesema yuko tayari kutuma wanajeshi nchini Libya, ikiwa Libya "itatoa ombi kama hilo".

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema, makundi ya wapiganaji kutoka Sudan na Chad walihusika katika vita nchini Libya mwaka huu.

Hata hivyo, ripoti hiyo haikuonesha kuwa wanajeshi wa Urusi walihusika katika vita hivyo.

Urusi imeendelea kukanusha madai kuwa, wanajeshi wake wameendelea kumuunga mkono wapiganaji wa upinzani Khalifa Haftar, ambaye kuanzia mwezi Aprili, amekuwa akijaribu kudhibiti jiji kuu Tripoli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.