Burkina Faso: Kanisa la Kiprotestanti lalengwa na shambulio Mashariki mwa nchi
Kanisa la Kiprotestani linaomboleza vifo vya waumini wake 14 waliouawa Jumapili Desemba 2 wakati wa ibada. Kanisa la Kiprotestanti katika mji wa Hantoukoura, mashariki mwa Burkina Faso lilivamiwa na watu waliojihami kwa silaha wasiojulikana.
Imechapishwa:
Makundi ya kijihadi yameonyeshewa kidole cha lawama kwamba yanaendelea kuhatarisha usalama kwenye sehemu za ibada.
Vitendo vya makundi ya kijihadi kushambuliwa sehemu za ibada vimeongezeka.
Shambulio hilo liliendeshwa na "watu waliojihami kwa silaha za kivita," kwa mujibu wa chanzo cha usalama, kilichonukuliwa na shirika la Habari la AFP. Waumini, ikiwa ni pamoja na mchungaji wa kanisa hilo na watoto, "waliuawa kikatili," chanzo hicho hicho kimebaini.
Katika taarifa yake, ofisi ya gavana imebaini kwamba "vikosi vya ulinzi na usalama" vimetumwa "kutoa msaada kwa watu waliojeruhiwa."