Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Utekaji nyara Burkina Faso: Wafanyakazi 4 wa shirika la mawasiliano ya simu Huawei waachiwa huru

Wafanyakazi wanne wa shirika la mawasiliano ya simu Huawei waliokuwa wametekwa nyara mwishoni mwa juma lililopita na kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni magaidi nchini Burkina Faso, wameachiwa huru.

Wafanyakazi wanne wa Huawei waliotekwa nyara kwenye barabara ya Ouo-Sidéradougou kusini mwa Burkina Faso wamachwa huru, Novemba 22, 2019.
Wafanyakazi wanne wa Huawei waliotekwa nyara kwenye barabara ya Ouo-Sidéradougou kusini mwa Burkina Faso wamachwa huru, Novemba 22, 2019. Google maps
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Usalama mjini Ouagadougou wamesema watu hao wanne, wafanyakazi wa kampuni ya simu ya China, Huawei waliokuwa wamepotea mwishoni mwa juma lililopita katika mazingira yenye kutatanisha wamepatikana jana jumapili wakiwa salama, taarifa ambayo pia imethibitishwa na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, vikosi vya ulinzi na usalama vya Burkinafaso vimefahamisha kuwa miongoni mwa wafanyakazi hao wa Huawei, mmoja ni raia wa China, wawili wakiwa raia wa Burkinafaso.

Wanne hao walipatikana saa ishirini na nne baadaye, katika operesheni ya kijeshi huko Ouagadougou, na baadaye walipokelewa na waziri mkuu Paul Kaba Thieba, raia Wachina, alikabidhiwa kwenye ubalozi wa nchi yake, imeongeza taarifa hiyo.

Watu hao walikamatwa na watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa ni magaidi ijumaa jioni, wakiwa katika shughuli za kufunga mitambo ya mawasiliano katika ofisi za Wizara ya Maendeleo na Uchumi katika eneo lenye usalama mdogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.