Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MACHAFUKO-USALAMA

Ethiopia: Serikali inajaribu kuweka udhibiti katika jimbo la Amhara

Mkoa wa Amhara nchini Ethiopia unakabiliwa na hali ya sintofahamu. Baada ya vifo vya watu zaidi ya 20 kati ya mwishoni mwa mwezi Septemba na mapema mwezi Oktoba, wakuu wa mkoa huo wametishia kuomba jeshi la nchi hiyo kuingilia kati ili kurejesha utulivu.

Katika moja ya mitaa ya Lalibela, katika mkoa wa Amhara, kaskazini mwa Ethiopia, Februari 2, 2019.
Katika moja ya mitaa ya Lalibela, katika mkoa wa Amhara, kaskazini mwa Ethiopia, Februari 2, 2019. © REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Machafuko katika eneo hilo la kaskazini mwa nchi yameendelea kushuhudiwa kwa karibu miaka mitano.

Mamlaka imeripoti vifo vya watu 22 tangu mwishoni mwa mwezi Septemba, kulingana na taarifa iliyotolewa na Baraza la Usalama la Mkoa wa Amhara.

Baraza hilo limezungumzia machafuko hayo kama machafuko makubwa katika ngazi ya kitaifa, vifo, nyumba zilichomwa, mali zilizoharibiwa na uchumi ambao umevurugika kwa kiasi kikubwa. Mzozo wenye vyanzo mbalimbali, ambao unaweza kuongezeka, Baraza la Usalama la Mkoa wa Amhara limebaini.

Baraza hilo limetangaza kuchukuwa hatua kadhaa: wananchi wa kawaida wamepigwa marufuku kumiliki silaha, makundi ya usalama yasiyojulikana rasmi yamepigwa marufuku na wananchi wametolewa wito wa kuwafichua wahalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.