Pata taarifa kuu
GUINEA-USALAMA-SIASA

Guinea yaendelea kukumbwa na mvutano wa kisiasa

Viongozi wakuu wa kitaifa kwa ajili ya ulinzi wa katiba nchini Guinea wameendelea kusalia korokoroni. Takriban viongozi 6 walikamatwa tangu Jumamosi iliyopita, mpaka leo mawakili wao wanasema hawafahamu walipo.

RAis wa Guinea, Alpha Conde
RAis wa Guinea, Alpha Conde ©FREDERICK FLORIN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa serikali wanasema hatua hiyo imekuja baada ya wito uliotolewa na viongozi hao wa kuandamana hii leo Jumatatu Oktoba 14 kupinga uwezekano wa rais Alpha Conde kuwania muhula wa 3.

Abdourahamane Sanoh mmoja miongoni mwa viongozi wanaopinga uwezekano wa rais Conde kuwania muhula wa 3 anasema viongozi waliozuiliwa hawana kosa lolote.

FNDC imeitisha maandamano makubwa hii leo jijini Conakry kupinga hatua ya rais Alpha Conde kutaka kuwania muhula wa 3.

Ingawa katiba ya Guinea inaruhusu tu mihula miwili mfululizo kuwa madarakani, Rais wa sasa wa nchi hiyo Alpha Conde, hivi karibuni alitangaza kwamba ana nia ya kugombea urais kwa muhula wa tatu mfululizo. Ili kusaidia kufanikisha hilo, Alpha Condé aliwataka wafuasi wake kutokubali wafuasi upinzani kufikia madaraka. Katika uchambuzi uliochapishwa na gazeti la Horizon Guinée, mwandishi wa bahari Sonny Camara anayeishi Conakry (mji mkuu wa nchi hiyo), aliripoti sehemu za hotuba ambayo Rais alihutubia tarehe 24 Machi, 2019:

"Nitakuwa ninavua kofia yangu ya Urais. Nitavaa kofia ya uanaharakati kwa sababu sasa niko tayari kupambana dhidi ya watu hawa [katika upinzani] […] mwe tayari kukabiliana […] Hakuna mtu yeyote katika Guinea atakayenizuia kuwauliza watu wangu wanachokitaka [kwa ajili ya nchi] […] Kama [Upinzani] wanataka kushinda kirahisi, muwe tayari kuwashinda ili wajue hamuogopi kitu chochote.

Conde alichaguliwa kuwa Rais wa Guinea mwaka 2010. Ni Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia katika historia ya nchi hiyo. Hata hivyo, uchaguzi wa mwaka 2010 ulikuwa na malalamiko kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi ikiwepo kituo cha Carter ambapo ililipotiwa kuwa karibu kura milioni moja zilipotea katika uhesabuji wa mwisho. Conde alichaguliwa tena mwaka 2015 kwa asilimia karibu 58 ya kura zote

Miezi michache baada ya kuchaguliwa mwezi Mei 2015, Condé alianza kupendekeza nia yake ya kugombea muhula wa tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.