Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Raia DRC wakaribisha serikali mpya, upinzani wakosoa

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imepata serikali mpya, miezi saba tangu kuapishwa kwa Rais Felix Tshisekedi. Serikali hiyo inakabiliwa na changamoto chungu nzima hasa katika kupambana na rushwa na umasikini na ugonjwa wa Ebola unaoendelea mashariki mwa DRC.

Ikulu ya rais, Kinshasa, DRC (Picha ya kumbukumbu).
Ikulu ya rais, Kinshasa, DRC (Picha ya kumbukumbu). ©Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa Kinshasa wamepongeza kuweko na serikali ambayo ina sura mpya na hasa vijana. Lakini upinzani umekosoa serikali hiyo wakibaini kwamba hawakushirikishwa katika serikali hii mpya.

Majimbo yote 26 yamewakilishwa kwenye serikali hiyo. Miongoni mwa mawaziri waliokuwa kwenye serikali ya Kabila na waliobahatika kurejea kwenye serikali hii mpya ni pamoja na Azarias Ruberwa waziri wa majimbo na Thomas Luahaka waziri wa elimu ya vyuo vikuu.

Katika serikali hiyo mpya,Chama cha rais wa zamani Joseph Kabila kimechukuwa wizara muhimu zikiwemo sheria, ulinzi, fedha na akiba.

Muungano wa FCC, wa rais wa zamani, Joseph Kabila umepata mawaziri 42, wakiwemo wale wa Sheria, ulinzi, fedha, madini, akiba na mipango ya serikali, huku muungano wa CACH wa rais Tshisekedi ukishikilia wizara ya mambo ya ndani, wizara ya mambo ya nje na bajeti.

Serikali hiyo mpya inamawaziri 66 pamoja na waziri mkuu. Rais Tshisekedi alichelewesha kutangazwa kwake kutokana na kwamba alitaka kuwapo na waziri anayewawakilisha walemavu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.